Tamasha la kuombea Uchaguzi Mkuu litakalofanyika katika mikoa 26 linatarajiwa Kuanza Jijini Dar-es-Salaam Juni 21, 2025
Akizungumza na waandishi wa Habari April 12, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion , Alex Msama amesema tamasha hilo halitakuwa na kiingilio ili kila mtanzania aweze kushiriki kwenye kuliombea taifa huku maandilizi yakiwa yanaendele vizuri
Msama ameongeza kuwa tamasha litaanzia katika mkoa wa Dar es salaam na kwenda mikoa mingine na limehusisha Wachungaji, Maskofu wa mikoa mbalimbali katika kuhakikisha wanaombea amani kulekea uchaguzi Mkuu.
Aidha amesema waimbaji mbalimbali wakubwa kutoka nje ya nchi na Ndani ya nchi watakuwepo kwenye tamasha la Kuombea Uchaguzi Mkuu Mwaka huu Wa 2025.

Comments
Post a Comment