Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Tra Yavunja Rekodi ya Makusanyo Kwa Miezi 9 Mfululizo yakusanya Trilioni 24.05


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanikiwa kukusanya Sh. Trilioni 7.53 katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2024/25, sawa na ufanisi wa asilimia 101.32 ya lengo la kukusanya Shilingi Trilioni 7.43.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda imeeleza kuwa ufanisi wa makusanyo ya Robo ya Tatu ya mwaka 2024/2025 ni sawa na ukuaji wa asilimia 13.47 ukilinganisha na kiasi cha Shilingi Trilioni 6.63 zilizokusanywa katika kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2023/24. 

Taarifa hiyo inaeleza kuwa ​makusanyo yaliyokusanywa katika robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2024/25 yanapelekea TRA kuweza kuweka rekodi ya kipekee katika utekelezaji wa majukumu yake kwa kufikia na kuvuka lengo la makusanyo kwa miezi 9 mfululizo katika mwaka wa fedha 2024/2025.

Taarifa ya Bw. Mwenda inafafanua kuwa katika kipindi cha mwezi Julai – Machi, mwaka wa fedha 2024/25, TRA imekusanya kiasi cha Shilingi Trilioni 24.05 sawa na ufanisi wa asilimia 103.62% ya lengo la kukusanya Shilingi Trilioni 23.21, na ukuaji wa asilimia 17.01 ukilinganisha na kiasi cha Shilingi Trilioni 20.55. 

Aidha, makusanyo hayo ni ya kiwango cha juu kabisa kufikiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kipindi kama hicho toka kuanzishwa kwake, na ni sawa na ongezeko la asilimia 77 toka kiasi cha Shilingi Trioni 13.59 zilizokusanywa katika kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2020/21, miaka minne toka Mhe. Dkt. Samia suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aingie madarakani.

Ufanisi huu katika makusanyo uliofikiwa mwezi Julai – Machi mwaka wa fedha 2024/25 ni matokeo chanya ya kutekeleza kwa vitendo maagizo na maelekezo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yanayohusiana na uongezaji wa uhiari wa ulipaji kodi kupitia uboreshaji wa huduma kwa walipakodi na uboreshwaji wa shughuli za biashara nchini.

Katika taarifa hiyo Bw. Mwenda anataja hatua zilizochukuliwa na kufanikisha ufanisi huo wa makusanyo kuwa ni pamoja na kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais la kuhamasisha ulipaji Kodi wa Hiari nchini.

Hatua nyingine amesema ni  kuongezeka kwa utendaji kazi mzuri, nidhamu na ubunifu kazini kwa watumishi wote wa TRA kwa kuendelea kuimarisha mahusiano na ushirikiano na Jumuiya za wafanyabiashara pamoja na wafanyabiashara wote nchini  na Kuendelea kutoa elimu ya kodi kwa njia mbalimbali kwa wafanyabiashara wote nchini.

Pia kuanza matumizi ya Mfumo wa Usimamizi wa Forodha (TANCIS) ulioboreshwa, uliozinduliwa mwezi Januari 2025, ili kuimarisha usimamizi wa vyanzo vyote vya mapato vya Forodha na Kufuatilia kwa ukaribu hali ya ufanyaji biashara nchini kwa kusimamia kikamilifu uzalishaji wa viwandani na matumizi  mashine za kielektroniki (EFD) nchini.

Hatua nyingine ni kuendelea kuweka kipaumbele katika utoaji wa huduma bora zinazozingatia mahitaji ya walipakodi, kuwahudumia walipakodi siku za mapumziko (Jumamosi na Jumapili) kupitia ofisi zote za TRA nchini na kuendelea kuboresha mahusiano na wafanyabiashara na kutatua changamoto za biashara kwa kutenga siku ya Alhamisi ya kila wiki kuwa ni siku maalum ya ‘Kusikiliza Walipakodi’ kupitia ofisi zote za TRA nchini.

Hatua nyingine ni kuendelea kutekeleza mikakati na kampeni za uhamasishaji wa uhiari wa ulipaji kodi nchini na Serikali kuendelea kuimarisha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji nchini, hali iliyopelekea Kuongezeka kwa shehena ya mizigo inayoingizwa au kuondoshwa nchini.

Pia Kuendelea kuongeza mahusiano baina ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na wawekezaji kupitia njia za majadiliano na mikutano na Kuendelea kuongezeka kwa idadi ya Waendesha Uchumi Walioidhinishwa (Authorized Economic Operators) nchini.

Bw. Mwenda katika taarifa yake anaeleza mikakati iliyowekwa na Menejimenti ya TRA ili kuhakikisha miezi iliyosalia kukamilisha mwaka wa fedha 2024/2025 wanavuka malengo ya makusanyo kuwa ni Kutekeleza maagizo yote ya Mhe. Rais.

Kukamilisha ujenzi wa moduli zote za Mfumo wa Usimamizi wa Kodi za Ndani (IDRAS) ifikapo Juni 2025, Kuendelea kuimarisha mahusiano na ushirikiano na walipakodi kupitia utoaji wa huduma bora pamoja na kampeni za elimu kwa mlipakodi.

Pia kuendelea kuimarisha usimamizi wa utoaji wa risiti za kielektroniki za EFD nchini kupitia kampeni mbalimbali za uhamasishaji, pamoja na kuwakumbusha wananchi juu ya umuhimu wa utoaji wa risiti za kielektroniki za EFD kwenye maendeleo ya nchi.

Aidha Bw. Mwenda ametaja mkakati mwingine kuwa ni Kuendelea kusimamia na kuimarisha misingi ya mfumo mzuri wa kodi, ikiwemo Haki na Usawa katika utozaji kodi (no favouritism or victimization) ili kuweka mazingira ya biashara yaliyo sawa na Kushirikiana kwa kikamilifu na timu iliyoteuliwa na Mheshimiwa Rais inayofanya mapitio ya mfumo wa utozaji kodi nchini ili kuleta maboresho.

Kuimarisha na kusimamia weledi (professionalism) na huduma nzuri kwa walipakodi (customer service) ikiwemo watumishi wetu wote kuvaa vitambulisho muda wote wanapotoa huduma.

Pia TRA itaendelea Kuimarisha vitengo vya Ukaguzi na Uchunguzi wa Kodi ili Kuzuia ukwepaji kodi za ndani na Forodha na kuondoa upotevu wa mapato ya Serikali ili kuweka mazinigira ya biashara yaliyo sawa kwa wafanyabiashara wote.

Bw. Mwenda katika taarifa yake amewashukuru Walipakodi kwa kuendelea kulipa Kodi kwa hiari na kuiamini TRA.



Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...