Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi ametua Uwanja wa Ndege wa Masasi, mkoani Mtwara, akiwa safarini kuelekea Tunduru, mkoani Ruvuma, tayari kuanza ziara yake ya siku 5. Uwanjani hapo, Balozi Nchimbi amepokelewa na viongozi wa Chama na Serikali, wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mtwara, Ndugu Saidi Musa Nyegedi.
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.








Comments
Post a Comment