Mbunge wa Ilala Mussa Azzan Zungu ameshiriki kwenye Ibada ya changizo maalum la maendeleo ya Kanisa la Waadventista Wasabato Magomeni.
Mhe Zungu ambaye pia ni naibu Spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano Tanzania alitumia nafasi hii kuwapongeza na kuwaomba waumini wa Kanisa la Wasabato waendelee kuliombea Taifa letu pamoja na Rais Mhe.Dkt . Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuliongoza Vema Taifa letu.
Amewaomba pia kuombea uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwaka huu uweze kufanyika kwa amani.













