Mbunge Mathayo Awatembelea Wahanga Musoma Mjini

GEORGE MARATO TV
0


Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini Mhe Vedastus Mathayo Leo 28/03/2025 amewatembelea wahanga wa mvua ilionyesha juni 23 na kusababisha maafa makubwa katika mitaa ya mjini, Manispaa ya Musoma Mkoani Mara. 

Mhe Mathayo amewapa pole watu wote waliofikwa na athari ya mvua na kuwaomba kuwa watulivu huku serikali ikianza kuyafanyia kazi Mambo mbalimbali ikiwemo kuwalipia Wananchi waliokuwa  wapangaji kwenye miji iliyokumbwa na ghasia hiyo ili waendelea na maisha kama kawaida.

Mbunge huyo kwa kushirikiana na mamlaka za serikali wikaya na mkoa wamechukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha wananchi hao wanapata msaada na kuendelea na maisha yao kama kawaida.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye ni mfaraji namba moja ametoa milioni mia moja kwa ajili ya wananchi 300 waliokubwa na janga hilo huku kamati ya maafa ofisi ya waziri mkuu ikiendelea na tathimini ili kujua ukubwa wa tatizo hilo na hatua za kuchukua.

Katika tukio hilo nyumba za wananchi,baadhi ya shule za msingi,miundombinu ya umeme na simu zilibomolewa na mvua hiyo iliyoambatana na upepo mkali.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top