Polisi katika Kaunti ya Nyamira nchini Kenya wanamsaka Kevin Onsombi mwanamume mwenye umri wa miaka 32 ambaye amempaka rangi mbwa wake ili aonekane kama Chui.
Hatua hiyo ya Onsombi ililenga kuwatisha maafisa wa kukusanya Marejesho ya mkopo baada ya kukosa kulipa mkopo wa Ksh 50,000.
Inasemekana Onsombi alikopa mkopo huo kutoka kwa Savings Sacco ili kulipia mahari ya mkewe ambapo alitoweka nyumbani kwake baada ya kubaini kugundulika kwa njama yake.
