Makamu Mwenyekiti Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amewahakikishia wananchi Wasira Awahakikishia Wananchi Tunduma Kupatikana Ufumbuzi Kero ya Msongamano Tunduma na mkoa wa Songwe kwa ujumla kuwa serikali ina fhamira ya dhati kutatua changmoto zao hususan ya maji na upanuzi wa barabara.
Wasira ameeleza hayo leo Machi 15, 2025 alipokuwa akiwahutubia wananchi mjini Tunduma, wilayani Momba Mkoa wa Songwe ambapo amesema kwa upande wa kero ya msongamano wa malori katika mji huo ufumbuzi utatokana na kupanuliwa kwa barabara ya Mbeya-Tunduma kuwa ya njia nne.
Amesema atakutana na Waziri wa Miundombinu (Abdallah Ulega) na atamfikishia ombi la wananchi wa mkoa huo kutaka upanuzi wa barabara hiyo ambao tayari umeanza mkoani Mbeya uwe na wakandarasi wawili ambapo mwingine aanzie Tunduma kuelekea Mbeya na hatimaye wakutane katikati kwa lengo la kuongeza kasi ya ujenzi.




Comments
Post a Comment