George Michael Uledi!
GAZETI la Mwananchi la March 16,2025 limebeba kichwa cha habari "Wasomi na VETA Mjadala Mkali"!Pia Jana mtandao wa Jamii Forum ulikuwa na mada kama hiyo kuhusu kauli ya Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa!
Kwanza kabisa napenda kumpongeza Mh Waziri Mkuu kwa kutoa kauli ya kishujaa sana japo imekuwa "NGUMU kumeza" kwa "wasomi" wetu!Ukweli unabaki kuwa tatizo la ajira sio la Tanzania tu bali lipo Kenya, Uganda,Malawi Afrika Kusini na hata Marekani pia!
Takwimu zinaonyesha kuwa sekta binafsi ndio mwajiri Mkuu Nchini Tanzania kwa sasa kuliko sekta ya Umma na "trend" hii itaendelea hivyo hivyo kwa miaka mingi ijayo!Sekta binafsi hasa katika "ubunifu" ndio itakuwa inazalisha ajira nyingi zaidi kuanzia sasa na kuendelea!
Juzi nilikuwa nawaona Vijana wa (NETO) waalimu WASIO na AJIRA wakilumbana na Serikali ili iwapatie ajira!Je,vipi kuhusu makundi mengine yakija na madai kama hayo?Nikawa nawaza kwamba Serikali Ina uwezo kwa kutoa ajira hizo kwa waalimu wote Nchini?
Kuna sehemu Serikali tuliteleza sana kiasi kwamba tukafungua Vyuo Vikuu kila kona ya Tanzania!Songea Mbeya Bukoba, Tanga,Mtwara na ikawa sasa kila Mkoa una "University"Dah!Sio kitu kibaya kuwa na Vyuo Vikuu kila kona lakini KOSA kubwa ambalo tulifanya ni kusahau kutanua Elimu ya kati(Technical Ed)!
Mahitaji ya ajira kwa mfano kwenye Sekta ya Madini (Mining) yanakuwa kila kukicha lakini hakuna watalaam wa KUTOSHA huko lakini pia kila kukicha migodi inafunguliwa Nchini kwetu!Vijana wengi hawajaona hii fursa ya ajira!
Nenda kwenye sekta ya ujenzi ajira nazo ni nyingi lakini hatuna watalaam wa "technical level" wa KUTOSHA badala yake mtu mmoja anajikuta anafanya KAZI zaidi ya moja kwenye mradi hivyo kusababisha Miradi mingi ya barabara mfano kuchelewa kuisha au kuwa chini ya kiwango!
Mh Waziri Mkuu amekuja na "proposal" ya kimkakati sana!Kuliko kukaa nyumbani na "degree" zako,kuliko "graduates" kuendelea kuendesha boda boda na Bajaj nadhani ni vyema vijana wetu wangetafuta ujuzi mwingine nje ya degree zao kwa lengo la kuajirika!
Ukifanya utafiti mdogo tu mfano kwenye sekta ya ufundi wa Magari(Gereji)vijana wengi wanaofanya KAZI huko"technical jobs" ni darasa la saba na form four lakini wanaishi maisha mazuri sana kuliko "graduates" wengi ambao wameajiriwa kwenye ajira RASMI!Mfano,Mkoani Mbeya eneo la Soweto Gereji limeajiri vijana wengi wenye Elimu ya VETA na wanaishi maisha mazuri sana mitaani!
Bahati mbaya sana "graduates" wetu wengi bado wapo kwenye usingizi mzito huku miaka inakwenda mbele na matokeo yake ni kulaumu Serikali kwamba hatuna ajira!
Ushauri!
Serikali lazima ije na programu Maalum kwa ajili ya "graduates" wetu ili waweze kuajirika katika maeneo mengine!Degree HAIWEZI kuleta ugali nyumbani lakini ujuzi unaweza kuleta mkate nyumbani!
Kauli ya PM Majaliwa ndio iwe uelekeo wetu kama Nchi kwa sasa!

Comments
Post a Comment