Na Shomari Binda-Musoma
MBUNGE wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo amepanga kuanza kuendesha harambee awamu nyingine kuchangia ujenzi wa shule za sekondari.
Awamu hii harambee hizo zitaanza kuanzia machi 25 hadi 27,2025 kwenye vijiji 3 vilivyoanza ujenzi wa shule.
Kwa mujibu wa taarifa ya ofisi ya mbunge iliyotolewa leo machi 15,2025 imeeleza harambee ya kwanza itafanyika Nyabakangara sekondari Kijijini Nyambono
tarehe 25 machi 2025 kuanzia
saa 8 mchana
Harambee ya pili itafanyika Kataryo sekondari Kijijini Kataryo
tarehe 26 machi 2025 kuanzia
saa 8 mchana na kumalizia Musanja sekondari Kijijini Musanja
tarehe 27 machi 2025 kuanzia
saa 8 mchana.
Taarifa hiyo imeeleza lengo la Musoma Vijijini ni kila Kijiji kiwe na shule za msingi za kutosha
na kila Kijiji kiwe na sekondari moja na zipo sekondari mpya zitakazofunguliwa mwaka huu wa 2025
"Sekondari 3 zinazojengwa na serikali za vijiji vya Butata, Kasoma na Kurwaki
na znazojengwa na wanavijiji 3 katika vijiji vya Muhoji, Nyasaungu na Kisiwa cha Rukuba.
" Sekondari mpya zilizoanza kujengwa mwaka huu (2025) kwa nguvu za wanavijiji ni 6 ambazo ni Chitare sekondari, Kata ya Makojo,Mmahare sekondari Kata ya Etaro, Kataryo sekondari Kata ya Tegeruka,Nyabakangara Kata ya Nyambono,Mwigombe Tech, Kata ya Kiriba na Musanja sekondari Kata ya Musanja",imesema taarifa hiyo.
Aidha taarifa hiyo imesema fedha za Mfuko wa Jimbo
kila moja ya hizo sekondari sita (6) tayari imepewa saruji mifuko 150 na nyingine zimepewa nondo
Hadi sasa mbunge huyo ameshafanya harambee kwenye shule ya sekondari Chitare na kuchangia mifuko ya saruji 150 na wananakijiji kuchangia 50
Mmahare sekondari amechangia mifuko ya saruji 150 na wanakijiji wakichangia mifuko ya saruji 155 na Mwigombe Tech mifuko ya saruji wanakijiji wamechangia mifuko 182,mbunge mifuko 200 na familia ya Mashenene inajenga darasa.

.jpg)
.jpg)
Comments
Post a Comment