Na Shomari Binda-Musoma
MENEJA wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Mara mhandisi Vedastus Maribe ameitaja Wilaya Bunda kama vinara wa wizi wa taa za barabarani
Hayo ameyasema kwenye kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika kwenye ukumbi wa uwekezaji.
Amesema matukio ya wizi huo yamekuwa mengi kwenye Wilaya hiyo na kuomba vyombo vya dola kufatili wezi hao na kuwakamata.
Maribe amesema wamekuwa wakiunganisha miundombinu ya taa lakini kwa Wilaya ya Bunda kumekuwa na tatizo kubwa la wizi wa taa hizo zinazowasaidia wananchi.
Akizungumza kwenye kikao hicho mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi ameagiza kusakwa na kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria wezi wa taa za barabarani.
Amesema haikubaliki kuona wizi huo unaendelea kwa masrahi ya watu binafsi wasiopenda maendeleo.
Amesema serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za maendeleo lakini wapo wachache wanaotaka kukwamisha ambao hawawezi kuvumiliwa.
Mtambi amesema wizi ulioripotiwa hauwezi kuvumilika na kuagiza jeshi la polisi kuwasaka wezi hao na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
" Naagiza kusakwa kwa wezi hawa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ili hatua ziweze kuchukuliwa dhidi yao maana huu ni uhujumu uchumi.
" Taa hizi zinawasaidia wananchi hata kwenye shughuli zao za uchumi lakini watu wachache kwa masrahi binafsi wanataka kuturudisha nyuma lazima tushughulike nao",amesema.
Awali akiwasilisha taarifa yake meneja wa TANROADS mkoa wa Mara mhandisi Vedastus Maribe ameitaja Wilaya ya Bunda kuwa vinara wa wizi wa taa za barabarani.
Akichangia kwenye kikao hicho mbunge wa jimbo la Tarime vijijini Mwita Waitara ameomba taa zilizopo Bunda zihamishiwa Tarime vijijini kwa kuwa kunakofanyika wizi wa taa hawataki maendeleo.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo ametoa ushauri wa uwepo wa mafundi wa uangalizi wa taa hizo ili kuzifanyia matengenezo zinapozima.

.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
Comments
Post a Comment