Mwenyekiti Wa Ccm Rorya Akiri Kutoa Fedha Kwa Watendaji Wa Ccm Matawi Na Kata Kinyume Na Maelekezo ya Chama
Na Shomari Binda;Mara
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Wilaya ya Rorya Ongujo Wakibara amekili kutoa fedha kwa watendaji wa chama hicho kwenye semina iliyofanyika februari 20.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika kutoa ufafanuzi kwa kile kilichoandikwa mitandaoni hivi karibuni amesema alitoa fedha kwa mapenzi yake kwa watendaji hao.
Amesema siku ya semina hiyo alifika ukumbini jioni semina ikiwa tayari imemalizika na watendaji wakiwa nje ya ukumbi na waliponiona walirudi ndani nami kwenda kuwasalimia
Ongujo amesema kwa kuwa tangu achaguliwe hajawahi kukutana na watendaji hao hivyo baada ya kusalimiana aliwawezesha nauli ambayo hakutaja kiasi.
Mwenyekiti huyo amesema amekuwa na kawaida ya kuchangia na kutoa nauli Mara kadhaa na kama kuna kosa kufanya hivyo chama kitanipa maelekezo
" Mimi na mbunge tumekuwa tukichangia na kutoa fedha katika kusaidia chama sasa kama ni makosa yatatolewa maelekezo na chama mkoa.
" Yale yaliyoandikwa mitandaoni ni ya uongo na yana lengo la kuchafua lakini mimi kama Mwenyekiti ntaendelea kusimamia ilani hii ambayo nimeshikilia hapa:,amesema.
Ongujo amesema yale ambayo yanaendelea wilayani Rorya ndani ya chama yanatokana na wastafu ambao hakuwataja majina yao
Amesema tangu kwenye uchaguzi waliendesha kampeni kuhakikisha wanashindwa kwenye uchaguzi na ndizo vurugu zinazoendelea hadi sasa.
Ongujo ameitisha kikao hicho na Waandishi wa Habari baada ya hivi karibuni kudaiwa yeye na mbunge wa jimbo la Rorya Jafar Chege kuvuruga semina ya watendaji wa CCM wa Wilaya ya Rorya kwa kutoa fedha kiasi cha shilingi elfu 50 kwa kila mjumbe.
Nao baadhi ya wanacha.a wa CCM waliozungumza na GMTV wamesema Mwenyekiti huyo alipaswa kutolea ufafanuzi juu ya kauli ambayo amekuwa akiitoa juu ya kwamba hukuna mwanachama mwingine atakayechukua fomu ya ubunge jimbo la Rorya.

.jpg)
Comments
Post a Comment