Zoezi la Kijeshi kati ya Jwtz na Jeshi la Marekani lafungwa

GEORGE MARATO TV
0

 

Zoezi hilo hilo linalojulikana Justifed Accord ambalo lilizinduliwa rasmi Februari 10 mwaka huu, ikiwa ni ushirikiano uliopo Katika ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Jeshi la Marekani ili kujenga ushirikiano wa usalama kupitia mazoezi ya pamoja ya kijeshi.



Akizungumza Leo, 15, Februali 2025, katika kituo cha mafunzo Cha jeshi la Msata Mkoani Pwani, wakati wa kufunga mazoezi hayo Meja Jenerali Selemani Mzee ambaye amemuwakilsha mkuu wa majeshi Nchini Jenerali John Mkunda, amesema kuwa mazoezi ya ushirikiano wa kawaida ambayo huwa wanayafanya na Nchi rafiki.


Amesema mazoezi hayo ni kama sehemu ya ushirikiano endelevu wa kijeshi na usalama kati ya Tanzania na Marekani yamelenga kuboresha usalama wa Kanda na uwezo wa kulinda amani ambayo yatashirikisha vikosi vya ardhini vya Tanzania na Marekani ambayo yametoa uzoefu wa thamani Katika mbinu za kukabiliana na vifaa vya mlipuko vya kutengeneza,Ulinzi wa kijinsia, taratibu za uokoaji wa matibabu na ujumuishaji wa ndege zenye rubani Katika operesheni za amani.


"Mafunzo kama haya yanasaidia kuwajenga Askari wetu malengo makubwa kwa hawa askari wetu wawe na uelewa wa pamoja na waweze kukabiliana na changamoto yanazohitaji juhudi za kijeshi kuyatatua,"amesema.

Nae Kaimu Balozi wa Marekani, Andrew Lentz amesema amefurahishwa na ushirikiano huo ambao Jeshi la Merekani imefanya imefanya kazi kwa karibu na vikosi vya kijeshi na usalama vya Tanzania kukabiliana na ugaidi, kuhakikisha Ulinzi wa mipaka yake na kusaidia shughuli za Kimataifa za kulinda amani.









Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top