Mahakama Kuu Kanda ya Musoma imesema Kwa Sasa imepunguza Mgogoro Mingi ya Ardhi

GEORGE MARATO TV
0


 Na Ada Ouko, Musoma.

MAHAKAMA kuu kanda ya Musoma mkoani Mara imefanikiwa kupunguza ucheleweshwaji wa mashauri yanayotokana na migogoro ya ardhi kwa kufuata sheria na utaratibu unaosimamiwa na mabaraza ya ardhi na nyumba nchini.

Hayo yamebainishwa february mosi mwaka huu 2025 na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo Fahamu Mtulya, mara baada ya kumaliza kikao chake cha majumuisho na wadau mbalmbali wa sheria waliokuwa wakitoa elimu kwa jamii ikiwa ni moja kuelekea kumaliza wiki ya sheria wilayani hapa.

"Suala hili tumeligundua tangu mwaka jana 2024, na tukumbuke kuna msemo wa kisheria ambao unajulikana kwa wengi unaosema haki ikichelewa ni kama haki iliyonyimwa".amesema .

Amesema katika Halmashauri ya Musoma kuna mwenyekiti wa baraza la nyumba na ardhi mmoja sambamba na wilaya za Serengeti na Tarime hali inayopelekea gharama ya kuwalipa na kugharamia ujio endapo amri ya Mahakama kama haitaki Mwenyekiti wa Baraza la Musoma kusikiliza shauri hilo tena, na kwamba bajeti mara nyingi haimo kwenye taasisi zao na wizara ya ardhi ambapo mabaraza hayo yanawajibika. 

Amesema wilayani hapa kuna mwenyekiti mmoja wa baraza na kwamba pindi Mahakama hiyo inapotoa amri shauri husika litakaa bila kusikilizwa kwa muda mrefu kwenye mabaraza yao kwa sababu mabaraza hayo yana mwenyekiti mmoja na washauri wawili.

Awali alisema, baada ya kubaini tatizo la ucheleweshaji wa mashauri kwenye mabaraza ya ardhi na nyumba Jaji Mtulya alisema walipokea ushauri kupitia vikao vya usukumaji wa mashauri hayo kutoka kwa wenzao wa mabaraza hayo.

"Tunachofanya sasa hivi sisi Mahakama Kuu kanda ya Musoma ni kubadilisha maelekezo tulioyazoea ya kutaka shauri lirudiwe kwa mwenyekiti mpya na washauri wa baraza wapya lakini kwa kufuata sheria na taratibu zinazosimamia mabaraza hayo" amesema Mtulya.

Kwa Upande wake Wakili wa kujitegemea kutoka chama cha Mawakili Tanganyika(TLS) Daud Mahemba alisema ni vizuri mamlaka husika iwe na bajeti ili kuhakikisha amri za Mahakama zinatekekezwa kwa wakati.

"Ni vizuri wizara ya ardhi na nyumba iweze kulitazama jambo hilo na walau iwe inatenga bajeti ikitarajia kwamba kuna mazingira Mahakama kuu inaweza ikatoa amri kwamba shauri fulani lirudiwe na likasikilizwe mbele ya mwenyekiti mwingine hasa katika mazingira ambayo majaji wakiona ishara za upendeleo kwenye mwenendo wa shauri" amesema Mahemba.





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top