Serikali na Bunge Zaipongeza Benki ya Azania

GEORGE MARATO TV
0


 WAZIRI mkuu Kassim Majaliwa na bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania,wameipongeza Azania benki kwa mchango wake mkubwa katika jamii hasa kwa kukubali kudhamini tamasha la Bunge bonanza linalofanyika ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan za kupambana na magonjwa yasioambukiza.

Wa kwanza kutoa pongezi hizo ni wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembea mwendo wa kilometa tatu na kushuhudia michezo mbalimbali,waziri mkuu Kassim Majaliwa,amesema kuwa benki ya Azania imeonyesha kwa vitendo kuunga mkono juhudi za Rais Samia kwa kukubali kudhamini bonanza hilo kubwa.

Amesema uamuzi wa benki ya Azania kudhamini bunge kufanya bonanza hilo kubwa imeonesha wazi upendo wa benki hiyo wa kujali afya za watanzania na kwamba kufanya hivyo ni kuunga mkono juhudi za Rais Samia katika mapambano ya magonjwa hayo yasio ambukiza.

Amesema kuwa azania benki ni moja ya taasisi kubwa ya fedha nchini na imekuwa ikijitokeza kudhamini michezo mbalimbali hii ni kuunga mkono jitihada za Mh Rais kwa kuhamasisha michezo nchini na kwamba mbali na kujitangaza lakini inawezesha kuinua uchumi wa wananchi.

Kwa sababu hiyo ameipongeza benki hiyo kwa uamuzi wake huo hasa hatua ya utoaji wa mikopo kwa wajasiliamali huku akitoa wito kwa Watanzania kuiunga mkono benki hiyo.

Kwa upande wake spika wa bunge Tulia Ackson alizungumza katika hafla chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo katika viwanja vya Bunge,ameishuru azania benki kwa ushirikiano mkubwa na taasisi ya Bunge.

Amesema katika siku za nyuma benki hiyo imekuwa ikishirikiana na bunge kwa shughuli mbalimbali lakini kwa ufadhili wa bunge bonanza la mwaja huu umekuwa mkubwa kuliko kipindi chochote.

Kwa sababu hiyo spika Tulia amesema bunge linatoa shukrani za dhati kwa uongozi wa azania benki kwa mchango wake mkubwa kwa bunge na taifa kwa ujumla.

Ameongeza kuwa bunge litaendelea kushirikiana na azania benki katika nyanja mbalimbali huku akisema mwaka huu wa fedha uwe mwema kwa benki hiyo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa bunge bonanza Festo Sanga akizungumza baada ya kumalizika kwa mashindano ya bonanza hilo amesema udhamini wa benki hiyo katika bonanza hilo umefanya kuwa bora kuliko mabonanza yote ambayo yamewahi kufanywa na bunge hilo.

Nae mkurugenzi mtendaji wa azania benki bi Esther Mang'enya akizungumza baada ya kumalizika kwa bonanza hilo,amesema azania benki ni benki ya Watanzania hivyo wana kila sababu ya kudhamini bunge bonanza kwa kutambua umuhimu wa afya kwa Watanzania kama rasmalimali muhimu. 

Kwa sababu hiyo amelishuru bunge kuwapa nafasi hiyo na kusema uamuzi wa benki yake ni kurudisha sehemu ya faida kwa Watanzania.

Amesema benki yake inatoa huduma mbalimbali kwa jamii hivyo kuwaomba Watanzania kujiunga na benki hiyo kutokana na huduma wanazotoa.

Ametaja baadhi ya huduma zinazotolewa na benki hiyo kwa wafanyabiashara wakubwa,wakati,wadogo na makundi maalum yakiwemo ya wajasiliamali na wanawake.















Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top