Na Derek Murusuri, Kibaha, Pwani
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi Joyce Mapunjo ameihakikishia Menejimenti ya Mfuko huo ushirikiano wake ili kufikia malengo.
Bi Mapunjo alikuwa anaongea katika mkutano wake wa kwanza na Wakurugenzi na Mameneja Mfuko huo, mwanzoni mwa wiki hii, baada ya kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya ya Wadhamini PSSSF, Desemba 2, 2024.
“Niwahakikishie kuwa tutafanya vizuri zaidi, niko transparent na huwa sipendi majungu,” alisema na kuipongeza Menejiment ya Mfuko huo kwa kuwakutanisha Wakurugenzi pamoja na Mameneja wao, kwa mara ya kwanza toka Mfuko huo uanzishwe chini ya Sheria ya Hifadhi ya Jamii Kwa Watumishi wa Umma ya Mwaka 2018, wakakaa pamoja na kupitia mipango na bajeti zao pamoja.
Bi Mapunjo alimpongeza Mkurugenzi Mkuu na Menejimenti ya PSSSF kwa kikao kazi [retreat] kinachoasisi mpango wa mabadiliko na kusema kuwa alijisikia vizuri sana kuanza majukumu yake kwenye Mfuko huo katika kipindi muhimu cha kuanza safari ya mabadiliko ya kuuboresha Mfuko.
“Mkapa alikuwa anakwambia tafuteni stakeholders [wadau] na tulikuwa tunawatafuta ili watuambie wapi tunahitaji kuboresha. “Retreat ijayo muwa identify [wachague] stakeholders [wadau] na wakaribisheni katika retreat kama hii ili waongee.” Alisema.
Alisema taasisi zilizofanikiwa ni zile ambazo zilikuwa zinakutana na wadau wao mara kwa mara, “…kama mtawala, organizations [taasisi] zilizokuwa zinafanya vizuri, ni zile ambazo zilikuwa zinafanya interactions [zinajichanganya] na wadau wao.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul-Razaq Badru, amesema, “tumepokea maelekezo hayo kutoka kwa Mwenyekiti wetu na tunaanza kuyafanyia kazi mara moja ikiwa ni pamoja na kuongeza juhudi kwenye huduma za outreach, [kuwatembelea] wadau wetu na kuendelea kutoa elimu ya Hifadhi ya Jamii,” alisema Bw. Badru, katika mahojiano baada ya hafla hiyo.







Comments
Post a Comment