-Dua hiyo maalum ya kumombea Rais Samia imefanyika katika msikiti wa Masjidi- Fisabillah Kurwaki Kusoma vijijini
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Mhe.Ghati Zephania Chomete, Leo tarehe 10 Januari 2025 ameshiriki Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Masjidi-Fisabillah iliyoko Kijiji cha Kurwaki, Kata ya Mugango, Wilaya Musoma Vijijini mkoani Mara.
Swala hiyo ya ijumaa imekuwa maalum kwa ajili ya kumuombea Dua Maalum Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri na Viongozi wote wa Serikali pamoja na kuliombea amani na utulivu Taifa letu la Tanzania.
Aidha, Uongozi wa Msikiti huo umemuombea pia Dua Maalum Mhe.Ghati Zephania Chomete (Mb), Mhe.Prof.Sospeter Muhongo (Mb), pamoja na Wahe.Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Musoma Vijijini.
Mhe.Ghati Chomete, aliambatana na M/Kiti wa UWT Wilaya Musoma Vijijini (Bi.Jane Joseph Chongo) na Wahe.Madiwani wa Viti Maalum (Mhe.Kadogo Kapi na Mhe.Florah Magwa).
Mh Ghati amekuwa akishiriki shughuli mbakimbali za kijamii na zile za kidini zenye maslahi kwa Taifa.






Comments
Post a Comment