Afisa Uhifadhi Mkuu Catherine Mbena Mkuu wa Idara ya Mawasiliano - TANAPA akitoa elimu ya Uhifadhi na Utalii kwa umma kupitia Kipindi cha JIRANI cha Radio Crown iliyop jijini, Dar es Salaam leo Januari 06, 2025.
Mbali na elimu ya Uhifadhi na Utalii pia ameendelea kutoa msisitizo kwa watalii wa ndani na nje kufuata sheria, taratibu na miongozo ya kuwepo ndani ya Hifadhi za Taifa.
Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbas akiongea kwa njia ya simu kupitia kipindi hicho amesisitiza kuwa sheria, taratibu na miongozo ya kuwepo ndani ya Hifadhi za Taifa ifuatwe kwani uhifadhi ndio moyo wa utalii.
"Uhai wa wanyamapori wetu ni jambo la muhimu sana kwetu sisi sote Afrika. Hawa viumbe-pori pamoja na mazingira-pori wana yoishi si tu ni muhimu kwa sababu ni chanzo cha maajabu na kuvutia bali hivi ni vitu muhimu katika rasilimali zetu za asili na kwa mustakhabali wa maisha yetu na ustawi wetu…..” Hayati Mwl. Julius K. Nyerere 1961
Afisa Uhifadhi Mkuu Catherine Mbena, na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano - TANAPA akitoa elimu ya Uhifadhi na Utalii kwa umma kupitia Kipindi cha MORNING MAGIC ya Magic Fm 92.9 iliyopo jijini, Dar es Salaam leo Januari 07, 2025.