Mbunge wa Jimbo la Butiama na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Jumanne Sagini ameonesha kukerwa na kampuni zinazochelewesha ujenzi wa chuo kikuu cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere cha kilimo na Teknolojia kinachojengwa wilayani Butiama mkoani Mara.
Kwa sababu hiyo amezitaka Kampuni za Shabdong Hi Speed Dejian Group Co LTD na Comfix and Engineering LTD zinazotekeleza Mradi wa Ujenzi wa majengo ya Hosteli, Cafeteria, Maktaba na Utawala katika Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT) kukamilisha kwa wakati kama Mkataba unavyoelekeza.
Ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa katika Ziara yake ya Kutembelea na kukagua uendelezaji wa Ujenzi wa Chuo hicho katika Kampasi ya Oswald Mang'ombe kijiji cha Butuguri na Makao Makuu yaliopo BAIC Butiama.