Na Helena Magabe Tarime.
MBUNGE wa Jimbo la Tarime mjini Michael Kembaki katika kuelekea kufunga mwaka amesema ulinzi na usalama Tarime uko vizuri licha ya kuwa amekerwa na Mbunge wa Kurya Magharibi Nchini Kenya Matias Rhobi kuhamasisha katiba mpya nchini katika Jimbo lake na kuleta uchochezi kwa wananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake amesema kitendo cha mbunge huyo kuchochoe wananchi kudai katiba mpya akiwa kwenye sherehe aliyoalikwa na Moja ya mtia nia ,akihoji kwanini Mbunge hakufika na kudai kuwa hakuna maendeleo Tarime ,hakuna bara bara za rami ni kitendo ambacho kimemkera na ni uvunjifu wa sheria za Nchi.
Amesema Mbunge huyo anatakiwa kufanya maendeleo Nchini kwake hasa kwenye Jimbo lake ambalo yeye si mgeni anazijua bararabara za jimboni kwake zilivyo mbovu hasa njia ya Kehancha ambayo ilijengwa zaidi ya miaka ishirini iliyopita hakuna maendeleo aliyofanya na Bungeni kwake ni Mbunge Bubu ambaye haongelei Jimbo lake na hayuko kwenye rekodi ya vyombo vya habari .
Akiendelea kuzungumza amesema Katiba mpya sio kipaumbele cha wananchi wa Tarime bali wananchi wanahitaji maendeleo kama vile ,maji,umeme elimi,afya barabara na mahitaji muhimu hiyo katiba mpya anayowahamasisha wadai haitawasaidia kwani hata huko jimboni kwake katiba haijaleta majibu ya changamato zinazomkabili wananchi wake hivyo aache kuzungumzia vitu ambavyo haviingii akilini.
Ameiomba Serikali ya Kenya kumchukulia hatua mbunge huyo kwa sababu nchi ya Kenya ni jirani na ndugu hivyo asingependa kuona anasababisha mgogoro wa kudai katiba na kusabanisha uvunjifu wa amani baina ya nchi mbili ambazo zina mahusiano mazuri.
" Kwanza sis utamaduni wetu ni tofauti na wa nchi yao sisi tuna heshima si rahisi kutukana Kiongozi Kila mtanzania ana wajibu wa kuilinda heshima ya Nchi yake kule kwao wanatukana viongozi kwanza kura wanapiga kwa ukabila,huku sisi tunafata sifa asilete mambo yake ya kisiasa every day nikutia kauli ambazo hazina tija "alisema Kembaki
Aidha amesema hakuna mtia nia ayemnyima usingizi kwani maendeleo amefanya na wananchi Wana mkubali na katika sekta zote amezitendea haki kwa upande wa barabara ambayo alisema bomani hakuna rami amesema itapata rami karibia maeneo yote na kwamba mbali na kilometa 6 za rami zilizo kwenye mpango zimeongezwa nyingine 18 ambapo kata ya nyamisangura na Bomani zitapewa kipaumbele.