Tanzania Yashiriki Mkutano wa Pamoja wa Mabaraza Matatu ya EAC

GEORGE MARATO TV
0


Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeshiriki mkutano wa Pamoja wa Baraza la Mawaziri la Uchukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa, Baraza la Mawaziri wa Nishati na Baraza la Mawaziri wa Viwanda, Biashara, Fedha na Uwekezaji ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika kwa njia ya mtandao Novemba 27, 2025 jijini Dodoma. 

Mkutano huo, pamoja na masuala mengine umeainisha miradi ya kielelezo ya miundombinu kutoka nchi Wanachama, kujadili na kupitisha ajenda zinazotarajiwa kujadiliwa katika Mkutano Kazi (Retreat) wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa EAC utakaofanyika hivi karibuni.  Mkutano huo utajadili na kupitisha miradi ya Miundombinu ya Kimkakati ya Kikanda ambayo utekelezaji wake utapewa kipaumbele kwa kutafutiwa ufadhili wa rasilimali fedha.


Kwa upande wa Tanzania mkutano huo umehudhuriwa na naibu wawaziri kutoka sekta mbalimbali wakiwawakilisha Mawaziri, akiwemo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. James Kinyasi Millya (Mb), Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Patrobas Katambi (Mb.), Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mshamu Munde (Mb) Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Salome Makamba (Mb) na Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David M.Kihenzile (Mb) ambaye aliongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo.








Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top