NIT yashirikiana na UDART kutoa mafunzo kwa Madereva wa Mabasi ya mwendokasi

GEORGE MARATO TV
0


Na Prosper Makene

Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa kushirikiana na Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART) kimetangaza fursa ya mafunzo maalum kwa madereva wa mabasi ya Mwendo Kasi (BRT). 

Mafunzo haya yanalenga kuwandaa madereva wenye ujuzi wa hali ya juu wa kuendesha mabasi ya BRT, ili kutoa huduma bora kwa abiria na kuimarisha usalama barabarani.

Mafunzo haya ni ya siku kumi, kuanzia tarehe 24 Novemba hadi 5 Desemba 2025, na ada ya mafunzo imetangwa kuwa shilingi za Kitanzania 150,000. Madereva wanaotakiwa ni wale wenye sifa za msingi kama vile wenye leseni ya udereva Class C, umri wa kati ya miaka 25-50, na uzoefu wa miaka mitatu ya udereva.

Lengo kuu la mafunzo haya ni kuandaa madereva ambao watakuwa na uwezo wa kuendesha mabasi ya BRT kwa ufanisi na usalama, huku wakitoa huduma bora kwa abiria. Mafunzo haya ni fursa muhimu kwa wale wanaotaka kujipatia ujuzi wa kuendesha mabasi ya kisasa na kuboresha nafasi zao za ajira katika sekta ya usafiri nchini Tanzania.

Watakaopata mafunzo haya wataweza kupata fursa ya kuweza kufanya kazi katika mradi wa mabasi ya BRT na kupata fursa za ajira katika sekta ya usafiri ndani na nje ya nchi. Mafunzo haya ni hatua muhimu katika kuboresha ubora wa huduma za usafiri nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji, mafunzo haya yanalenga kuandaa madereva ambao watakuwa na uwezo wa kushughulikia mabasi ya BRT kwa ufanisi na usalama. Mafunzo haya yanajumuisha masomo ya nadharia na mafunzo ya vitendo, ili kuhakikisha kwamba madereva wanapata ujuzi wa kutosha wa kuendesha mabasi ya ya kisasa hususani mwendo kasi. 

Lengo ni kuhakikisha kwamba madereva wanapata mafunzo bora ambayo yatawasaidia katika kazi zao na kuboresha huduma za usafiri nchini Tanzania.

"wa wale ambao wamevutiwa na fursa hii, ni muhimu kujitokeza mapema na kujiandikisha kwa kufuata taratibu zilizowekwa na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji," amesema Afisa Mmoja Mwandamizi kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji. 





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top