Mbunge Mavunde Azindua Soko Dogo la Wafanyabiashara wa Mtaa wa Nzasa-dodoma Jiji

GEORGE MARATO TV
0


Mbunge wa Jimbo la Mtumba Mh. Anthony Mavunde leo asubuhi amefungua rasmi soko la wafanyabiashara wadogo la Mnyambugwe kwenye Mtaa wa Nzasa,kata ya Chihanga.

Soko hilo ambalo limejengea kwa ufadhili wa shirika la VSO linatarajiwa kuwa na wafanyabiashara zaidi ya 100 ambao awali walikuwa wanafanya biashara zao katika maeneo ya wazi na hivyo kuathiriwa na mvua na jua.

Akizungumza katika ufunguzi huo,Mbunge Mavundw amewashukuru wadau wa maendeleo VSO kwa ujenzi wa soko hilo la kisasa na kueleza kuwa ni mkakati wake kuhakikisha mitaa ya Jimbo la Mtumba inapata masoko ya aina hiyo ili kusaidia kuchochea uchumi wa maeneo hayo.

Mbunge Mavunde pia ameishukuru serikali chini ya uongozi wa Mh Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa mikopo isiyo na riba kwa wafanyabiashara hao ambayo imesaidia kuwaongezea mitaji ya kufanya biashara.

Mbunge Mavunde pia ameahidi kuwapatia meza wafanyabiashara hao za kuwekea bidhaa zao ili zitunzwe katika hali ya usafi.

Meneja Mradi wa VSO Ndg. Fortunatus Nyundo amesema shirika lake litaendelea kushirikiana na Wananchi wa Jimbo la Mtumba katika kuwawezesha miradi mbalimbali ya uchumi na ya kijamii.

Naye Diwani wa kata ya Chihanga Mh. Alice Kitendya amesema uwepo wa soko hilo la wafanyabiashara wadogo litasaidia upatikanaji wa bidhaa kwa wananchi kwa ukaribu zaidi na utachochea kukua kwa uchumo wa eneo la Nzasa.&







Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top