Majaliwa Awasili Shelisheli Kumwakilisha Rais Dkt. Samia Uapisho wa Rais Mteule Dkt. Patrick

GEORGE MARATO TV
0


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 26, 2025 amewasili Seychelles kwa ajili ya kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye uapisho wa Rais mteule wa sita wa nchi hiyo Dr. Patrick Herminie 

Tume ya Uchaguzi ya Taifa ilimtangaza Mheshimiwa Dkt. Patrick Herminie wa Chama cha United Seychelles (US) kuwa mshindi baada ya kumbwaga Rais aliyekuwa madarakani, Mheshimiwa Wavel Ramkalawan wa Chama cha Linyon Demokratik Seselwa (LDS). 

Mheshimiwa Dkt. Patrick Herminie alipata asilimia 52.7% ya kura, huku Rais Wavel Ramkalawan akimaliza wa pili kwa kupata 47.3% ya kura.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top