Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Bilionea Aidan Kuifufua Sunshine, Kiwanda Kikubwa Cha Kuchenjua Dhahabu Chunya

*Kitakuwa na uwezo wa kuchenjua tani 500 kwa Saa 24*

*Kuzalisha Ajira 350 kwa Watanzania*

*Ukarabati kuchukua  Miezi Miwili*


 *Chunya*

Septemba 2024, jina la Bilionea Aidan Andrea Msigwa lilitikisa Sekta ya Madini kama radi katikati ya jua kali kwa kuuza kilo 111.82 za dhahabu. Alivuna zaidi ya shilingi bilioni 20.11 kwa mkupuo mmoja hatua iliyotikisa si tu wadau wa madini, bali iliwaamsha Watanzania wengi hadi kuvuka mipaka ya nchi. Aidan hakutajwa tu kama gwiji wa madini, bali aliwekwa rasmi kwenye meza ya mabadiliko ya kiuchumi ndani na nje ya Tanzania.

Baada ya kuvuna mabilioni kutokana na kuuza dhahabu hiyo Aidan hakukimbilia anasa bali alichagua kuwekeza kwa watu baada ya kutumia kiasi kikubwa cha fedha kuinunua Kampuni ya SUNSHINE Group iliyoko Matundasi Chunya iliyokuwa ikimilikiwa na wawekezaji kutoka China. Kwa sasa yupo mbioni kwa kushirikiana na wawekezaji wengine wa China kukifufua kiwanda hicho kikubwa cha kuchenjua dhahabu kilichokuwa kimesimamisha shughuli zake kwa takribani miaka miwili. Kiwanda hicho kinatarajiwa kuchukua miezi miwili ya ukarabati baada ya taratibu za kiuwekezaji kukamilika. Aidha, kinatarajia kuchenjua tani 500 kwa saa 24, kuzalisha zaidi ya ajira 350 kwa watanzania huku kwa wageni zimetengwa nafasi 40 tu ambapo chini ya ubia huo, wanatarajia kuleta teknolojia.

Anasema mbali ya kuinunua SUNSHINE fedha nyingine aliwekeza kwenye ununuzi wa vifaa kwa ajili ya kuendeleza shughuli zake za uchimbaji na uchakataji madini kama ununuzi wa escavetor, magari na mitambo mingine ya kurahisisha kazi zake. Pia, Aidan ni mmiliki wa leseni kadhaa za uchimbaji mdogo wa madini na anazo leseni nyingine ambazo zina uzalishaji  lakini bado hajaanza kuchimba na anaweza kushirikiana na mwekezaji. Vilevile,  anao mtambo wa kuchakata dhahabu  wenye uwezo wa kuchakata tani Mia Mbili 200 kwa saa 24.

Hadithi ya Aidan si ya mtu mmoja kutengeneza mabilioni, bali ni simulizi ya kizalendo ya mtu kurejesha matumaini kwa mamia ya familia, vijana, na jamii zinazotegemea Sekta ya Madini kama chanzo cha maisha. Katika mahojiano maalum na timu ya Madini Diary,  amefunguka  juu ya safari yake, maono yake, na kwa nini anasema huu ni mwamko mpya wa kiuchumi na unaong’aa kama jua la asubuhi kwa Chunya na Tanzania .

Aidan anasema hakuwahi kufika sekondari. Elimu yake rasmi iliishia darasa la saba, lakini ndoto zake hazikuishia darasani. Tangu mwaka 1989, alihangaika kwenye machimbo, makarasha, kuchenjua, akijifunza kwa vitendo, akikosea na kujirekebisha, akipigania maisha kwa jasho la kweli la mchimbaji mdogo.

Lakini leo, licha ya kuvuna bilioni 20.11 za mkupuo na kipato kingine kutoka vyanzo vingine vya uchimbaji, anasema jambo moja analojutia ni kutokuendelea na shule. “Sasa hivi nikikutana na wageni kama hawa mnaowaona, nasemewa na wengine… hilo huwa linaniumiza sana kwasababu ningeweza kuzungumza mwenyewe. Hiki ni kitu ninachojutia kweli japo nilitamani kufanikiwa kwa haraka,” anasema kwa utani wenye uzito. Ndiyo maana licha ya mafanikio yake, anasisitiza kwa nguvu: “Usiache shule kwa tamaa ya mafanikio ya haraka. Mafanikio yatakuja, lakini elimu ni msingi wa kudumu’’, anasema Aidan.

Licha ya kuvuna bilioni 20.11 kwa mkupuo mmoja, Aidan Msigwa hakubadilika. Anasema wazi, “Mimi tarehe zote huzimalizia porini si mtu wa starehe, kuanzia tarehe 1 hadi 30, niko porini,’’.

Badala ya kupumzika, aliona mafanikio hayo kama hatua ya kwanza ya kuongeza bidii zaidi. Yalimwinua yakamweka mbele ya jamii kama mfano wa kweli, mtu wa kawaida aliyefanikisha ndoto kubwa kwa uvumilivu, uaminifu, na juhudi za kweli. Wengi sasa wanamchukulia kama kioo, wakiona ndani yake picha ya matumaini yao. Amewapa nguvu ya kupambana zaidi, na kwa kiasi kikubwa, amechochea wimbi jipya la uchimbaji na uwekezaji Chunya si kwa wachimbaji wadogo pekee, bali hata wawekezaji wa ndani na nje wanaotaka kuwa sehemu ya hadithi yake. Kwa Aidan alama aliyoiweka haitoshi anataka kwenda mbele zaidi na anasema wachimbaji wadogo wataleta mabadiliko Tanzania.


*Ombi kwa tasisi za fedha na Serikali*

Kutokana na mazingira ya shughuli za madini Aidan anatoa ombi kwa taasisi za fedha kuwaamini wachimbaji na wasipewe masharti sawa na wawekezaji wengine kutokana na uhalisia wa shughuli za madini. Pia, anatoa ombi kwa Serikali kutokuhesabu madeni ya nyuma  baada ya kuanzishwa utaratibu mpya wa kutozwa asilimia 2 za Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) katika yote Msigwa hakuacha kuishukuru Serikali kwa kuwezesha mazingira yaliyomfikisha alipo.

Na hii kwa ufupi ndiyo SIMULIZI ya Aidan Andrea Msigwa  mmiliki wa Kampuni ya Mdimi Investment, kutoka darasa la Saba hadi Bilioni 20.11: Safari ya uaminifu, uvumilivu na sasa SUNSHINE.  Simulizi zaidi ya Aidan ifuatilie hivi karibuni kupitia Madini Diary.




*Vision 2030: Madini ni Maisha na Utajiri*


 

Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...