Mara.
Wananchi wa Mkoa wa Mara wanatoa pongezi za dhati kwa Mheshimiwa Ghati Chomete,Mbunge wa Viti Maalum, kwa uongozi wake thabiti, ushujaa wa kisiasa, na moyo wa kujitoa kuwatumikia wananchi – hasa wanawake wa Mkoa wa Mara.
Mheshimiwa Ghati Chomete ameendelea kuwa mstari wa mbele katika kutafuta kura za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,kuwasemea wanawake wa Mkoa wa Mara na kuhakikisha kuwa sauti ya wanawake inasikika kwa nguvu katika majukwaa ya kisiasa.
Kupitia ziara zake, mikutano ya hadhara na vikao na makundi mbalimbali ya kijamii, ameendelea kusambaza ujumbe wa matumaini, umoja na ushindi kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na wagombea wake wote.
Uongozi wake umechochea ushiriki mpana wa wanawake kwenye siasa, ujasiriamali na maendeleo ya jamii kwa ujumla, na amekuwa daraja muhimu kati ya serikali na wananchi.
Kwa hakika, *Mheshimiwa Ghati Chomete* umeonesha mfano wa kuigwa kwa wanawake viongozi—mshindi wa mioyo ya wananchi kwa unyenyekevu, ushawishi na utendaji.
*Hongera sana Dada(Msubhati)Ghati Chomete… umeweza!*
Endelea kusimama imara, kutafuta kura kwa bidii, na kuibeba sauti ya wanawake wa Mkoa wa Mara bila kuchoka.
Umejitoa kwa nguvu zote kutafuta kura za CCM katika maeneo yote ya mkoa wa Mara ili kuhakikisha DKT SAMIA SULUHU HASSAN anapata kura za kishindo,Wabunge na Madiwani wanapata ushindi mkubwa,umeonesha mfano mkubwa katika kukipigania chama chako
*Kwa moyo na vitendo – CCM, Ushindi Daima!* 💚💛