*KATA YA HOMBOLO MAKULU-JIMBO LA MTUMBA*
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtumba kwa tiketi ya CCM Ndg. Anthony Mavunde ameendelea na awamu ya kwanza ya kampeni yake ya mtaa kwa mtaa kwa kila kata kuzungumza na makundi mbali katika maeneo husika.
Ndugu Mavunde ameendelea na ziara yake kata ya HOMBOLO MAKULU na kutembelea na kuzungumza na wananchi wa Mitaa ya ;
-𝙈𝙖𝙮𝙚𝙩𝙤
-𝙕𝙚𝙥𝙞𝙨𝙖 𝘼
-𝙕𝙚𝙥𝙞𝙨𝙖 𝘽
-𝙈𝙖𝙨𝙚𝙮𝙖
-𝙆𝙖𝙣𝙜𝙖𝙡𝙞𝙢𝙖
-𝙈𝙨𝙞𝙨𝙞
Ndg. Mavunde pia alitumia fursa hiyo kuwaombea kura Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt. Samia S. Hassan na Mgombea Udiwani wa kata ya Hombolo Makulu Ndg. Mokiwa Sahali.