Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu na Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China , Balozi Chen Mingjian na Ujumbe wake Ofisini kwake Dodoma.
Majadiliano hayo yalilenga kujadili mambo mengi ya ushirikiano baina ya Tanzania na China hasa katika maeneo ya ukuzaji ujuzi, maendeleo na mabadilko ya teknolojia duniani n.k
Kikwete amewahakikishia kuwa Tanzania itaendelea kuenzi uhusiano uliopo baina ya nchi zetu hizi na kuwa Tanzania itaendeleza uhusiano huu kwa kuimarisha maeneo yote ambayo yanakutanisha katika mashirikiano haya. Pia kuwashukuru serikali ya China kwa mabadiliko makubwa ambayo yanaelekea kukuza ujuzi kwa vijana wa Kitanzania na nia yao ya kufanya maonyesho makubwa ya kazi yanayolenga kufunua fursa za vijana wa kitanzania kujiajiri na kufungua milango ya kuajiriwa na makampuni makubwa ya kigeni yakiwemo ya China nchini hapa.








Comments
Post a Comment