Viongozi wa Tanzania waungana maonesho ya Dunia nchini Japan

GEORGE MARATO TV
0

 

Na Jovina Massano 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Masauni ameungana na ujumbe wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, katika ziara yao nchini Japan kushiriki Maonesho ya Dunia ya EXPO 2025 yanayofanyika Osaka, Japan.

Mei 25, 2025, ikiwa ni Siku ya Taifa la Tanzania (Tanzania National Day) katika maonesho hayo, ujumbe wa Tanzania umeendelea kuonyesha utajiri wa nchi katika sekta mbalimbali zikiwemo utalii, uwekezaji, teknolojia na utamaduni.

Ushiriki huu wa maonesho haya makubwa duniani unalenga kuitangaza nchi kimataifa, kuvutia wawekezaji na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa hususan katika sekta za maendeleo endelevu na mazingira.

Tanzania ni miongoni mwa mataifa yanayoshiriki kikamilifu katika EXPO 2025, ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kukuza diplomasia ya uchumi na kulinda mazingira.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya Siku ya Taifa la Tanzania katika Maonesho hayo.



Aidha Tanzania imeonesha nguvu katika utalii, mazingira, na fursa za uwekezaji  ikiwasilisha sura ya  taifa mbele ya dunia! 

Tukio hili linaendelea kuonesha dhamira ya Tanzania kushiriki kikamilifu kwenye majukwaa ya kimataifa kwa maendeleo endelevu.

              Mwisho

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top