Na Shomari Binda-Musoma
TAASISI ya Nasimama na Mama imejitambulisha dasmi kwa mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi tayari kwa kufanya kazi ya kusemea mazuri yanayofanywa na Rais Dkt.Ssmia Suluhu.
Viongozi wa taasisi hiyo wamejitambulisha jana mei 12,2025 ofisini kwa mkuu huyo wa mkoa baada ya kupokelewa na kufanya nae mazungumzo.
Akizungumza ofisini hapo,Mwenyekiti wa taasisi hiyo Cde.Ibrahim Assey amesema lengo la kuanzishwa kwa taasisi hiyo licha ya kumsemea Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kuifikia jamii yakiwemo makundi ya vijana,wanawake na makundi maalum na kuelezea fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo mkoa wa Mara.
Amesema zipo fursa kwenye sekta ya kilimo,uvuvi,elimu na ujasiliamali kupitia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri ambapo wananchi wanapaswa kupata uelewa wake.
Mwenyekiti huyo amesema ili kufikia malengo ya kuifikia jamii nakufikisha elimu wanahitaji kupata ushirikiano kupitia ofisi mbalimbali.
Amesema watahakikisha wanatekeleza majukumu yao pamoja na kusemea kazi nzuri inayofanywa na Rais Dkt.Ssmia Suluhu Hassan kwa kufika maeneo mbalimbali mkoani Mara.
" Tunakushukuru sana mheshimiwa mkuu wa mkoa kwa kutukaribisha na kutupokea ofisini kwako baada ya kukupa ujumbe wa kukutembelea.
" Lengo letu na kuanzishwa kwa taasisi yetu ni kusemea mazuri yanayofanywa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuifikia jamii pamoja na kuelezea fursa mbalimbali zinazopatikana mkoa wa Mara.
" Tunakushukuru mkuu wa mkoa kwa kuyupokea na tunakuahidi tutafanya kazi nzuri ya kuifikia jamii na kuelezea fursa zilizopo mkoani Mara",amesema.
Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi amewapongeza viongozi wa taasisi hiyo kwa maono yao ya kutaka kumsemea Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na kuifikia jamii.
Amesema ofisi yake itawapa ushirikiano kutokana na kuwa na mawazo mazuri ikiwa ni pamoja na kuifikia jamii na kuelezea fudsa zinazopatikana mkoa wa Mara.




Comments
Post a Comment