Milioni 70 Zaokolewa na Takukuru Mara yakiwemo Malipo ya Makaburi Hewa

GEORGE MARATO TV
0


Na Shomari Binda-Musoma 

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU) wa Mara imefanikiwa kuokoa kiasi jumla ya shilingi milioni 70,212,800.00 yakiwemo malipo ya makaburi hewa.

Hayo yamesemwa leo mei 27,2025 na Mkuu wa taasisi hiyo Muhamed Shariff alipokuwa akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi 3 ya januari hadi machi 2025 kwa Waandishi wa Habari.

Amesema katika zoezi la uhamishaji wa makaburi kwa wananchi wanaopisha upanuzi wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Kata ya Nyatwali Wilaya ya Bunda kiasi cha milioni 49,200,,200 kimeokolewa.

Mkuu huyo wa TAKUKURU amesema fedhà hizo iliyokuwa ilipwe kama kifuta machozi kwa wanufaika wa makaburi hewa 123 ambapo kila kaburi lllipaswa kulipwa shilingi 400,000.

Amesema walifanikiwa jambo hilo baada ya kufanya uchambuzi wa mchakato mzima uliotumika kuhalalisha ulipaji fidia za makaburi yaliyopswa kuhamishwa.

Amedai kuwa uchambuzi ulibaini katika hatua ya uthaminishaji makaburi hayo yalithaminishwa kwa namna yalivyotambulishwa na kuonekana kuwepo na sio kwa wathaminishaji kujilidhisha na kuwepo kwa miili ndani ya makaburi.

" Kwa kasoro hile tulishauri mamlaka ya ulipaji fidia ambao ni msimamizi wa mradi ( TANAPA Kanda ya Magharibi) isilipe fidia kwa makaburi ambayo hayataonekana kuwa na mabaki ya miili wakati zoezi la uhamishaji makaburi litakapokuwa linafanyika.

" Utekelezaji wa ushauri huo ndio uliowezesha kupatikana kwa makaburi hewa 123ambayo hatimaye wanufaika wake hawakulipwa fidia ya shilingi milioni 49,200,000",amesema.

Katika ufatiliaji wa mirafi ya maendeleo amesema wamedbhubiti shilingi milioni 21,012,800 za mradi wa ujenzi wa hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda unaotelezwa kwa ujenzi wa awamu ya pili

Fedha hizo zilikuwa zimetengwa na kuanzishiwa mchakato wa manunuzi ya vifaa vya ujenzi a.bavyo tayari vilishanunuliwa.

Aidha amesema katika ufatiliaji wa utekelezaji wa miradi 28 ya maendeleo yenye thamani ya bilioni 9,260,900,920.78 katika sekta ya Afya,Elimu,Barabara na Maji kati ya miradi hiyo miradi 12 yenye thamani ya shilingi bilioni 3,958,553,938.78 ilibainika kuwa na dosari.


Amesema kwenye program ya TAKUKURU Rafiki iliyofanyika Kata ya Kibasuka wilayani Tarime imefanikisha ukarabati wa josho la kuogeshea mifugo katika Kijiji cha Weigita ambapo awali wananchi walilalamikia josho hilo.

TAKUKURU mkoa wa Mara katika kipindi hicho cha miezi 3 imetoa elimu kwa umma huku katika kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu wananchi wameombwa kutoa taarifa juu ya matukio ya viashiria vyake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top