Na Richard Mrusha
Mwenyekiti was Taasisi ya Demokrasia na Maendeleo Tanzania Democracy and Devoloment,TADED) Chalilla Kibuda ibuda leo April 12,2025 amesema swala la uchaguzi mkuu ni jukumu la kila mtanzania mwenye sifa za kipoga kura.
Amesema wao kama Taasisi wamejipambanua kuhamasisha watu kujitokeza kwenye uchaguzi maana kwakifanya hivyo watapata maendeleo ambapo kuanzia ngazi ya kata Hadi Taifa.
Ameongeza kuwa Kwa kuhamasisha watu kushiriki katika uchaguzi utaofanyika Oktoba mwaka huu ni haki ya kila mtu na asitokee mtu yeyote wa kada yeyote na kuwavunja mioyo watu .
Kibuda amesema Katika uchaguzi huu ni haki ya kila mwananchi kushiriki katika kuchagua viongozi wataodumu kwa kipindi cha miaka mitano kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema Uchaguzi huu kwa katiba hii hakuna chombo chochote kinachoweza kuzuia kutofanyika uchaguzi ambapo hata chama kilichopo madarakani hakiwezi kufanya hivyo.
Ameongeza kuwa Hata hivyo katika maandalizi hayo yamefanyika vizuri ikiwemo wananchi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura nchi nzima.
Suala la kuzuia uchaguzi kwa Chama fulani kusema No Reform.No election ni jambo ambalo haiwezekani kuleta katikati ya zoezi hilo kuanza.
Hata hivyo tangu' tumefanya uchaguzi 2020 katika kipindi hicho walikuwa na nafasi ya kufanya juu ya kuliendea jambo la uchaguzi na serikali ikachukua hatua", amesema Kibuda.
Ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuweka utulivu wa Siasa amefanya mambo makubwa pamoja na kuwa na maridhiano ya kuruhusu mikutano kufanyika ambapo vyama vinaendelea kufanya mikutano bila vikwazo.
Aidha katika mazingira tulionayo nchi iko tulivu kabisa kila mwananchi anaendelea kufanya maisha yake hii inaonyeesha amani ambapo Rais na vyombo vyake kuendelea kuhudumia wananchi wake.
Hata hivyo katika suala siasa nchi iko salama na kufanya mataifa mbalimbali kuwekeza kwa kigezo kuwa na siasa salama (political Stability).
Nchi imeendelea kutekeleza miradi yote ikiwemo bwawa la umeme la Nyerere ambapo hadi sasa limekamilika ,ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR unaendelea.
Amesema kwenye sekta ya Utalii nchini watalii wamekuwa wakiongezeka hii inatokana na serikali ya Dkt.Samia Suluhu Hassa na kutengeneza filam ya The Royal Tour
Amesema Nchi imeendelea kujiimarisha katika mahusiano ya kimataifa kwa Rais kufanya ziara ambapo ndio matokeo yanayooneka katika uwekezaji nchini.
Amesema Katika Taded ya Waasa Wananchi Kupiga Kura iliyojiwekekea Taasisi ni pamoja na kufanya makongamano nchi nzima kwa kushirisha wasanii mbalimbali ambapo mazungumzo yao yanaendelea kufanyika na hawezi kuyatoa kwenye vyombo vya habari.


Comments
Post a Comment