Kikao cha ushauri cha mkoa wa Kagera kimeridhia kutenga maeneo maalum (viteule) katika mipaka yote ya mkoa huo na kumilikisha vikosi vya jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) ili kuimalisha usalama wa nchi na kupambana na wahamiaji haramu.
Mkuu wa mkoa huo Hajati Fatma Mwassa ameeleza hayo leo wakati akifunga kikao cha RCC kilichofanyika Manispaa ya Bukoba mkoani humo kikiwa na agenda mbili kupitia na kuridhia bajeti ya mwaka 2025/2026 pamoja na kuwasilishwa mapendekezo ya kujenga uwanja mpya wa ndege wa mkoa wa Kagera.
Anasema wameridhia kwa pamoja kuongeza viteule maeneo ya mipaka ya mkoa huo mazungumzo tayali yameanza na wakuu wa Wilayani zote saba pia kule kwenye ngazi za vijiji ili maeneo yote ambayo ni ya kimkakati kwenye ngazi zile yanakatwa na kumilikishwa kwa jeshi letu la ulizi la wananchi kulinda nchi yetu.
"Kikao hiki tumekubaliana kwamba kupitia kamati za usalama ngazi zote kudhibiti uhamiaji haramu wawe wanatoka nje ya nchi au ndani wasiingie Kagera bila taratibu hii agizo linatokana na kwamba tumegundua kule ngazi za vitongoji na vijiji kuna shida sana.
Aidha wameagiza taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa (TAKUKURU) mkoa huu iongeze udhibiti wa viongozi na watumishi wanaokula rushwa na kuingiza wahamiaji haramu lakini pia, Serikali tumeishaiomba kusimamisha kutoa vibari kwa watu wanaokuja kulima vijishamba vidogovidogo eti mtu ana hekari tano analeta mtu kuja kumlimia vibari vya hivi kutolewa uhamijia RCC ya Kagera tumekataa.
Aidha ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kagera imeweka utaratibu wa kutoa motisha kwa watu wanaotoa taarifa sahihi na za kweli kuhusu wahamiaji haramu.
Piusi Ngeze ni mwenyekiti mstaafu wa chama cha Mapinduzi na mzee maarufu mkoani Kagera amesema vyombo vipo vya ulinzi na usalama hivyo washirikiane na wananchi kuwadhibiti wahamiaji haramu kwani hiyo si jambo la kumsubiri Rais Samia Suluhu Hassan aje kwani hii siyo vita.







Comments
Post a Comment