Na Mwandishi Wetu , Korogwe
RAIS wa Jamhuri ya Muungano, Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa ahadi kwa wananchi kuwa atailea Tanzania kwa kusukuma mbele maendeleo kwa kuanzisha na kuibua miradi mikubwa yenye tija na maendeleo kwa nchi.
Rais, aliyasema hayo jana wakati akiweka jiwe la msingi la bwawa la umwagiliaji lililopo Tarafa ya Mkomazi, wilayani Korogwe ambapo alisema kuwa anatoa ahadi kuwa atahakikisha anasukuma mbele maendeleo ya wananchi katika sekta mbalimbali
"Ahadi yangu kwenu kama mama nitaendelea kuilea Tanzania kama mtoto wangu, nitaendelea kusukuma miradi ya jamii yote inayotakiwa kuwepo, maji, Umeme, afya, elimu, kilimo nitajitahidi kufanya kazi yangu kama inavyotakiwa hiyo ni ahadi yangu kwenu," alisema Rais Dkt Samia.
Alisema bwawa la Mkomazi ambalo awali Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitamani kulitengeneza lakini hakufanikiwa vivyo hivyo kwa Marais wa awamu tofauti nao hawakujaliwa kutokana na Hali ya uchumi, lakini serikali yake imeweza.
Alisema kuwa Tanzania inakwenda kuwa nchi ya kilimo kupitia mradi ya ujenzi wa mabwawa ya umwagiliaji inayoendelea Kwa Sasa nchini.
Alisema kuwa Kwa Sasa nchi inauwezo wa kujitosheleza Kwa chakula takribani asilimia 128 lakini nchi jirani zinazotuzunguka zinakabiliwa na uhaba wa chakula hivyo kupitia ujenzi wa mabwawa itasaidia kuongeza kiwango Cha uzalishaji wa chakula na hivyo kuuza nchi za jirani.
Alisema kuwa ndio maana serikali inakwenda na sera ya Kuwawezesha vijana kushiriki katika shughuli za kilimo Ili waweze kushiriki kwenye fursa hiyo kwani soko la uhakika lipo tayari.
"Hili bwawa Ili kuwa ni ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere lakini haikiweza kutimizwa kutokana na hali za kifedha na awamu nyingine hivyo hivyo lakini awamu hii tumeweza kupata afuani ya kifedha na tumeweza kutekeleza mradi huu "alisema Rais Samia.
Alisema lengo la serikali kutoa fedha zaidi ya bilioni 900 kwa ajili ya mradi huo na bwawa jingine la Kidunda lililopo karibu na Dar es salaam ni kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kilimo cha uzalishaji wa mazao ya kilimo baada ya nchi kujitosheleza kwa chakula kwa zaidi ya asilimia 128.
"Kwa hiyo kuna soko kubwa sana nje ya nchi zinazotuzunguka na huko ndiko tunataka kuwaelekeza vijana wetu na mabwawa hayo yamejebgwa kwenda kuongeza eneo la kilimo lakini na wananchi wataweza kuvuna maradufu kwa mwaka mmoja," alisema.
Alisema wanakwenda kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kilimo kama ambavyo Marehemu Mwl Nyerere alisema kilimo ni uti wa Mgongo hivyo wanaonesha kwa vitendo.
Amewataka wananchi wa eneo lonakojengwa bwawa hilo katika kata ya Mkomazi kuhakikisha wanashirikiana na wakandarasi kuhakikisha hawachukui vifaa vya ujenzi na mkandarasi akamilishe kwa wakati.
Kuhusu mashamba ya mkonge yaliyotelekwzwa kama ambavyo wabunge wawili Timotheo Mnzava wa Korogwe Vijijini na Dkt Alfred Kimea walivyoomba kwa Rais yafutiwe hati, Rais amemwagiza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Deogratias Ndejembi kukaa na Timu yake kufanya tathimini ya mashamba ambayo hayaendelezwi waone cha kufanya.
Alisema anajua kwamba yapo baadhi ya mashamba yamekopewa nje ya nchi lakini serikali haiwezi kuona mtu mmoja anaweka rehabi Ardhi ya nchi kwa manufaa yake.
"Waziri na timu yako fanyeni tathimini mashamba mengine ambayo hayafanyiwi kazi japo baadhi wametakopea nje lakini hatuwezi kumruhusu mtu mmoja aweke reheni mashamba yetu kaaeni mfanye tathimini na mniletee tuamue kwa pamoja," alisema Rais.
Waziri wa Kilimo Husein Bashe alisema kuwa skimi mbili za Mkomazi na Chekeli zitawanufaisha wananchi zaidi ya 2000 kutoka katika kata Saba za Jimbo la Korogwe Vijijini.
Mapema asubuhi Rais, alizindua jengo la utawala la halmashauri ya Bumbuli ambako aliagiza watumishi wote walitumie jengo hilo kutoa huduma kwa wananchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Bumbuli Baraka Zikatimu alisema jengo hilo lililojengwa kwa awamu nne hadi kukamilika kuanzia mwaka 2018, limetumia shilingi bilioni 5.575.
Pia Rais Dkt Samia, akiwa mjini Lushoto kwenye mkutano wa hadhara
Vile vile ametangaza kumrejesha nyumbani Mbunge wa Bumbuli na Waziri wa zamani, Januari Makamba takribani Miezi sita sasa tangu kumuondoa kwake kwenye Baraza la Mawaziri, "Mwanangu nilimpiga kikofi, nikamfichia chakula sasa leo namrudisha nyumbani kwa Mama"
Rais Samia amenukuliwa akisema "Mwanangu Januari arudi kwa Mama, sisi wamama mnatujua ukimkera mama anakupiga kikofi, anakufichia chakula si ndio? Sasa mwanangu nilimpiga kikofi, nikamfichia chakula lakini leo namrudisha kwa Mama." Amesema Rais Samia.
Bila kutaja sababu ya 'kumchapa kibao', kumuadhibu kwa kumuondoa kwenye baraza la Mawaziri katikati ya mwaka 2024, baada ya maneno yake hayo alikumbatiana na Januari Makamba, mtoto wa kiongozi mstaafu wa serikali na wa Chama Cha Mapinduzi, Mzee Yusuph Makamba na baadaye kushuhudiwa shambwe na makofi kutoka kwa wananchi waliokuwa wakishuhudia tukio hilo.













Comments
Post a Comment