MISA Tanzania yawatembelea wadau wa habari, Kanda ya Ziwa

GEORGE MARATO TV
0



Mwandishi wetu ;Mwanza



Mwenyekiti wa MISA Tanzania Bwana Edwin Soko Leo amefanya ziara kwenye Taasisi za Kitaifa zenye Makao Makuu Kanda ya Ziwa zikiwemo Mamlaka ya Uthibiti wa  Nishati na Maji(EWURA) Kanda ya Ziwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Kanda ya Ziwa.

Soko amekutana na Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandishi Imelda Salumu  na kujadilili nama ya kufanya kazi Kwa pamoja likiwemo eneo la kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari kuelekea uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu ili wafanye kazi Kwa weledi zaidi.

Kwa upande wake Mhandishi Imelda alieleza kuwa anaipongeza  MISA Tan Kwa kuona umuhimu wa kuwa karibu na wadau mbalimbali wa habari na  kusisitiza ataendelea kufanya kazi pamoja na wanachama wa MISA na waandishi wa habari wote nchini.


Wakati huo huo Soko alikutana pia na Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa George Mhina ambapo walijadili juu ya umuhimu wa MISA  Tan kwenye kusimamia weledi ndani ya taaluma ya habari.


Mhina alisema kuwa, EWURA wapo tayari kushirikiana na MISA Tan kwenye kufanya kazi kitaaluma ili kusaidia kupatikana  kwa habari jengefu.


Ziara hizo zimekuwa ni mwendelezo wa Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika(MISA TAN) kujitambulisha Kwa wadau na kuongeza uwigo wa kufanya kazi Kwa pamoja.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top