Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga leo Disemba 29, 2024 ametembelea vituo vitatu (3) vya watu wenye mahitaji maalumu vilivyopo katika wilaya ya Babati ikihusisha; Kituo cha kulelea wazee magugu,Kituo chakulelea Watoto wenye ulemavu unaotibika cha Zilper na kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi mazingira magumu cha Hossana na kutoa zawadi za sikukuu ya mwaka mpya 2025.
RC Sendiga ameeleza kuwa zawadi hizo zimetoka kwa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni ishara ya upendo wa Mhe. Rais kwa wananchi hao katika sikukuu hizi za Mwisho wa Mwaka.
Zawadi zilizotolewa zilihusisha Mchele, Mafuta ya kupikia, Sukari, Unga wa ngano, Viungo, Sabuni, juisi, maji, Mbuzi, madaftari na kalamu.
Aidha, RC Sendiga amesema zoezi hilo la ugawaji wa zawadi kwa vituo hivyo linaendelea katika Wilaya zote za Mkoa wa Manyara.