Taasisi ya The Angeline Foundation imekabidhi vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuunga mkono juhudi mbalimbali anazozifanya Mhe Dkt.Angeline Mabula Mbunge wa Jimbo la Ilemela kwa kutoa vifaa na ufadhili Kwa watoto wanaoishi mazingira magumu pamoja na Yatima
Akipokea vifaa hivyo katika Bonanza la Krismass lililofanyika kwenye viwanja vya Furahisha Katibu wa Mbunge Ndugu Charles David ameshukuru taasisi ya The Angeline Foundation ambayo imekuwa ikifanya kazi kubwa sanaa kuunga mkono jitihada mbalimbali za Mhe Mbunge katika kuwatumikia wananchi.
Pamoja na hivi vifaa ambavyo siku ya leo tunavipokea n kuvitoa Kwa vijana hawa zaidi ya 50 ambao wanasoma Kwa ufadhili wa Mhe Dk Angeline Mabula Mbunge wa Jimbo la Ilemela leo tunapokea vifaa hivi Kristmass Bonanza ikiwa ni msimu wake wa nane tangu kuanzishwa Kwa taasisi hii imekuwa ikifanya kazi kubwa kutoa vifaa mashuleni , vifaa vya afya pamoja mahitaji mbalimbali .
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Ndugu Ayubu Bariana mratibu kutoka taasisi hiyo Alisema
" Kwa kipindi Cha Miaka 8 sasa Tunaendelea kufanya Krismass Bonanza ikiwa na lengo la kutoa Burudani Kwa wananchi wa Jimbo la Ilemela lakini pia kama ishara ya kuunga mkono jitihada na kazi kubwa alizozifanya na anazoendelea kuzifanya Mhe Mbunge wa Jimbo la Ilemela tangu Kuingia kwake madarakani