Mkuu wa Mkoa Kagera atoa Zawadi ya Xmass kwa Watoto wa Mazingira Magumu

GEORGE MARATO TV
0


 Na Angela Sebastian ;Bukoba 

MKUUU wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa ameunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya tendo la uhuruma kwa watoto yatima,wanaoishi mazingira magumu na wenye uhitaji katika sikukuu ya Christmas.

Hajat Mwassa amewaalika watoto zaidi ya 200 kutoka katika vituo vinne vya kulelea watoto yatima na wale wenye uhitaji vilivyoko Manispaa ya Bukoba ambapo amepika chakula na kisha kula nao mlo wa mchana lengo,likiwa ni kusherehekea sikukuu hiyo muhimu ili nao wajione kuwa wanayo haki ya kuungana na wengine wakati wa furaha.

"Nimeamua kupika mwenyewe hapa Ikulu ndogo ya mkoa wa Kagera kisha kupakua,kula na kunywa na watoto hawa wenye uhitaji na yatima ili tufurahi wote katika sikukuu hii,maana tumezoea kubeba vyakula,nyama na vinywaji kupeleka vutuoni na kuacha lakini mimi nimeona tendo hilo la huruma nilitekeleze kwa njia hii"ameeleza Mwassa 

Kwa upande wa mwenyekiti wa cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bukoba Manispaa Joas Zachwa amempongeza Hajat Mwassa kwa kuandaa hafla hiyo na kuwapikia chakula watoto hao na kula nao kwamba ameonyesha upendo na hekima kubwa kwani watu wamezoea kununua nyama na vyakula na kupeleka nyumbani kisha kula na watoto wao.

"Wewe umeamua kula na hawa wahitaji huu ni kuonyesha upendo mkubwa kwa wanakagera hata wewe ungeamua kukaa na familia yako ila umeonyesha ni jinsi gani una upendo wa kweli na watu hasa hawa vijana hivyo CCM inakupongeza na kukushukuru sana maana huu ni utekelezaji wa Ilani yetu pia umeonyesha tabia aliyojijengea Rais wetu Dk. Samia Suluhu Hassan ya kufanya matendo ya huruma kwa kusaidia wahitaji kama hawa"amesema Zachwa 

Anasema wananchi wa Wilaya ya Bukoba na mkoa mzima wana amani na kazi unazofanya za kuleta maendeleo hivyo zinaonyesha taswira ya Rais Samia ya kuteua watu makini,wenye upendo na huruma kwa Watanzania kwahiyo Mungu atawalipa yaliyo mema

Naye Mwenyekiti wa jumuiya ya vijana wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kagera (UVCCM) Faris Burham amesema mkuu huyo wa mkoa amefanya tendo la huruma na lenye baraka ambalo limewagusa watoto ambao pia ni vijana hivyo ni tendo la kuigwa na kila mmoja kwani limekuwa la kipekee kwasababu haijawahi kutokea watoto hao wenye uhitaji kukaribishwa Ikulu ndogo na kupikiwa,kuhudumiwa chakula na mkuu wa mkoa na kujumuika nao.

Baadhi ya watoto waliopata mlo huo walishukuru na kupongeza upendo wa dhati aliouonyesha Hajat Mwassa kwao na kumuomba aendelee kuwakumbuka pia apeleke salamu zao kwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan. 

 Rewina Pius Paulo kutoka Nusuru yatima kata Kashai Manispaa ya Bukoba ni mmoja watoto hao ambapo anasema, wao hawakupenda kukosa wazazi bali ni mapenzi ya Mungu hivyo wanamshukuru Rais Dk.Samia kwa huruma yake anayoonyesha kwa Watanzania wenye mahitaji mbalimbali ambapo pia ametoa shukrani pia kwa mkuu wa mkoa Hajat Mwassa kwa upendo alioonyesha kwa watoto hao.









Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top