JESHI la polisi mkoani Kagera limepiga marufuku disco toto wakati wa sikukuu za Christmas na mwaka mpya kwasababu kumbi zinazotumika hazina viwango vinavyotakiwa hivyo, atakayetaka kuendesha zoezi hilo apate kibari cha polisi baada ya kuwafanyiwa ukaguzi na kujilidiisha.
"Kwa wale wanaopenda kuendesha disco toto polisi Kagera tumepiga marufuku kwasababu mara nyingi wanaoendesha disco kwa ajili ya watoto hawazingatii uwezo wa kumbi zao, tumeishashuhudia katika baadhi ya maeneo tumepoteza watoto wengi japo siyo Kagera "anaeleza kamanda Chatanda
Amesema tukio kama hilo liliwahi kutokea kule mkoani Tabora miaka ya nyuma ambapo watoto wengi walipoteza maisha na sababu ilikuwa ni uzembe kwasababu mmiliki alichokua anangalia ni kupata fedha na si usalama wa watoto.
"Kwa yule ambaye anadhani anaweza akakidhi vigezo aje polisi twende tukague tujiridhishe kama eneo linafaa na liwe eneo la wazi na kuhakikisha kuwa halina viashiria hivyo,mpaka saaa sijapata mtu yoyote mwenye eneo lenye sifa za kuendesha disco toto hivyo ni marufuku"ameagiza Chatanda.
Amewataka wananchi kutoacha nyumba wazi kwasababu polisi hawawezi kulinda nyumba mojamoja kwasababu waharifu wanaweza kutumia mwanya huo kuiba.
"Watoto watoke wakiwa na waangalizi hata humu barabarani tunakemea waendeshaji wa vyombo vya moto wasiendeshe wakiwa wamelewa ili kuepusha watoto wetu kuwa waanga wa ajali zisizotarajiwa,mtoto akiwa peke yake barabarani kuna uwezekano wa kupatwa na janga hilo"anaeleza RPC
Pia ametaadhalisha waendesha vyombo vya moto kuwa makini na kufuata sheria ili kuepusha watoto kuwa wahanga wa matukio ya ajili,pia amewataka wazazi kutowaacha watoto kuzurula ovyo wa sikukuu hizo wahakikishe wana mtu mzima amabaye atawaongoza hasa wanapokwenda kutembelea fukwe zilizoko pembezoniwa ziwa Victoria.
Aidha Kamanda Chatanda amesema kesi 22 za kubaka zilifikishwa mahakamani kwa kipindi cha Januari hadi Desemba mwaka huu,ambapo watuhumiwa sita wa makosa hayo wamehukumiwa kifungo cha maisha jela huku watuhumiwa 16 wakihukumiwa miaka 30 jela.
Pia watuhumiwa nane wa kesi za ulawiti nao wamehukumiwa kifungo cha maisha ambapo watuhumiwa 14 wa kesi zilizohusisha watoto wadogo walioko chini ya umri kisheria na wanafunzi wamehukumiwa kulipa faini,kuchapwa viboko na kifungo cha nje ambapo kesi nne wamehukumiwa vifungo mbalimbali kutokana na makosa waliyoyatenda.
Amesema wamafanikiwa kupunguza ajali za barabarani ambapo kwa mwaka 2023 ajali zilikuwa 57 na mwaka huu ni 45,madereva 259 walifikishwa mahakamani ambapo kati yao 63 wamafungiwa leseni,178 walipewa adhabu ya kulipa faini na madreva tisa wa magari makubwa walifungiwa leseni.