Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda anasikitika kutangaza kifo cha Meja Jenerali Martin Shuminzi Busungu(Mstaafu) kilichotokea Desemba 24 Mwaka huu, Majira ya Saa kumi na robo za Jioni.
Katika Utumishi wake Jeshini,Jenerali Busungu aliwahi Kushika Madaraka Mbalimbali yakiwemo Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Mwaka 2018 hadi 2019.
Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Gaudentius Gervas Ilonda imeeleza kuwa Taarifa za Utoaji wa heshima za mwisho kwa marehemu pamoja na shughuli za mazishi zitatolewa baadaye.