MRATIBU wa kampeni ya msaada wa kisheria ya Rais Dkt, Mama Samia Legal Aid Mkoani Mara amesema Serikali imeanzisha mchakato wa kupunguza kesi zinazotokana na migogoro ya ardhi Mahakamani.
Buliro amesema hayo hivi karibuni , wakati akitoa elimu ya sheria mbalimbali ikwa ni sheria za ardhi, mirathi, unyanyasaji wa kijinsia kwa wakazi wa mtaa wa Mtakuja "A" kata ya Mwisenge Manispaa ya Musoma
"tayari tumepewa maelekezo na wizara ya katiba na sheria tufanye uchunguzi ili kubaini tatizo lakini suala la uhaba wa mwenyekiti pia laweza kuchangia na njia pekee ya kupunguza mashauri ya ardhi ni kuongeza wenyeviti wa mabaraza, walau kila wilaya awepo mwenyekiti mmoja"amesema.
Wakili wa kujitegemea kutoka chama cha mawakili Tanganyika Emmanuel Werema alisema mwenyekiti mmoja wa mabaraza ya ardhi anahudumia mashauri 2000 endapo akipatwa na changamoto ya kiafya au kifamilia kesi itasogezwa miezi ya mbele.
Aidha alisema mwenyekiti huyo anatoa huduma katika mabaraza ya Musoma mjini, Musoma vijijini na Butiama na kwamba katika kipindi cha nyuma alikua akifika wilaya za Serengeti na Bunda kutoa huduma kwa wananchi.
"Mwenye wajibu wa kuongeza wenyeviti ni msajili wa mabaraza wakishauriana na waziri wa ardhi na Nyumba kwa sababu mabaraza hayo hayapo chini ya Mahakama" alisema Werema
Awali Abasi Shabani Mkazi wa eneo hilo aliuliza swali kwa nini kumekuwa na msongamano wa mashauri hayo, kwa kuwa familia yake ilifungua kesi ya ardhi tangu mwaka 2019 jully
" Kuna namna mwenyekiti wa baraza wanapaswa kutenda haki mfano kesi yangu ilisikilizwa upande mmoja na kutolewa hukumu bila upande mwingine kuwepo, Kesi yangu ni kati ya Rukia Mkangara shangazi yangu dhidi ya Kalumba Shabani kaka yangu" amesema.
Kwa upande wake muundaji wa mkutano huo mwenyekiti wa mtaa huo Aloyce Masatu lengo la mkutano huo ni kuwafikishia wananchi elimu ya sheria karibu ili watambue haki na wajibu wao.
sambamba na hilo alitoa shukrani kwa wakazi wa mtaa huo kwa kumchagua kupitia chama cha mapinduzi(ccm) kuwa mwenyekiti wa mtaa huo.
Kampeni hiyo imeweza kuwasaidia wananchi wasioweza kumudu gharama za mawakili wamepewa wanasheria bure ambao wamewasimamia Mahakamani, na kwamba jumla ya vijiji 270 mkoani hapa vilifikiwa na huduma hiyo.