Mwauwasa kujenga visima viwili na kuboresha mtandao wa maji Ngudu

GEORGE MARATO TV
0

 

MRADI MPYA KUIMARISHA HUDUMA YA MAJI NGUDU 

*DC KWIMBA AIPONGEZA WIZARA YA MAJI* 

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) imeanza utekelezaji wa mradi wa ufufuaji Visima Viwili na Uboreshaji wa Mtandao wa Maji kwa KM 4.5 unaolenga kunufaisha wakazi wa mji wa Ngudu Wilayani Kwimba kwa kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji.

Akizungumza wakati wa zoezi la mapokezi ya Shehena ya kwanza ya bomba yenye urefu wa KM 1.5, Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija ameshukuru Serikali kupitia Wizara ya Maji kwa kutekeleza ahadi kwa wakati na kusimamia nia ya Mhe. Raisi ya kumtua mama ndoo ya maji kichwani.

"Tumekuwa na changamoto ya uchakavu wa bomba kuu linalosafirisha maji kutoka chanzo cha Ihelele na kuhudumia Mji huu na Wizara kupitia Mhe. Waziri Jumaa Aweso aliahidi kutafuta mbadala wa haraka kwa mpango wa muda mfupi, tunaona leo mmetekeleza na kazi imeanza, nawapongeza kwa kubuni mradi huu na nawasisitiza MWAUWASA mfanye kazi hii kwa bidii ili ikamilike kwa wakati ninawaamini". Amefafanua Mhe. Ludigija.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA Neli Msuya amesema Mradi huo utakaogharimu kiasi cha TZS Milioni Mia tatu (300,000,000.00) utawezesha uzalishaji maji kwa Lita 600,000 kwa siku kutoka katika Visima na kupunguza changamoto ya uhaba wa maji. Alisema kwa bomba la Maji linalotoa maji chanzo cha KASHWASA cha Ihelele linawezesha mji huo kupata lita 600,000 kwa siku wakati mahitaji halisi ni lita milioni 1.2 kwa siku.

Aidha, Mkurugenzi Neli ameshukuru Mbunge wa Jimbo la Kwimba Mhe. Shanif Mansoor kwa ushirikiano wake tangu hatua ya kubuni Mradi na kuongeza kuwa Mradi unatarajiwa kukamilika mwezi Februari 2025. "Fedha za utekelezaji wa mradi tayari tumepatiwa na Waziri na kazi iliyobaki ni ya utekelezaji," alisisitiza.

Akieleza kazi zitakazotekelezwa katika Mradi huo, Meneja wa Miundombinu MWAUWASA Mha. Stanley Mwasawala amesema Mradi utajumuisha ulazaji wa bomba jipya la usafirishaji maji kutpka katika chanzo hadi kwenye matenki kwa urefu wa KM 4.5, Ufungaji wa Pampu 3 za kuzalisha na kusukuma maji, Ufufuaji wa Visima viwili eneo la Kiliaboya, pamoja na ukarabati wa miundombinu chakavu katika chanzo hicho kilichoanza kutumika tangu mwaka 1955 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top