Mkuu wa Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi, Meja Jenerali Idd Said Nkambi amewatunuku vyeti wa hitimu wa Astashahada na Stashahada katika fani ya Teknolojia ya Elektroniki na Mawasiliano ( Basic Certificate and Diploma in Electronics and Telecommunication Technology) katika shule ya Kijeshi ya Ulinzi wa Anga( SKUA) Mkoani Tanga Leo tarehe 05 disemba 2024
Akizungumza katika mahafari ya nne kwa ngazi ya Astashahada na ya tatu kwa ngazi ya Stashahada , Jenerali Nkambi amewataka wahitimu kutumia elimu waliyopata kwa manufaa ya Jeshi na Taifa.
Aidha Mkuu wa shule Kanali Abel Paul Mbai amepongeza jitihada zilizofikiwa na kueleza kuwa mchakato unaendelea kuhakikisha wanaanza kutoa elimu ya Shahada kuanzia mwakani 2025.
Amewashukuru wadau ambao wamekuwa na mchango mkubwa kwa uongozi wa shule katika kuandaa mitaala .




Comments
Post a Comment