Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete, leo amewakabidhi tiketi za safari kwa vijana 26 kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini wanaokwenda kwenye programu ya mafunzo kwa vitendo nje ya nchi.
Vijana hao watakwenda nchi za Ujerumani, Sweden, na Denmark,kupitia programu inayowezeshwa na Taasisi ya CRDB Bank Foundation kwa kushirikiana na Ushirika wa Wajasiriamali Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUGECO)