RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dr Samia Suluhu Hassan ametangaza kuunda tume mbili kuchunguza malalamiko ya wakazi wa Ngorongoro mkoani Arusha.
Rais Samia ametangaza uamuzi huo leo Desemba mosi 2024 katika Ikulu ndogo ya Arusha, wakati akizungumza na Viongozi wa jamii ya Kimaasai inayoishi katika eneo hilo la Ngorongoro kwa lengo la kuwasikiliza baada ya kuwepo kwa baadhi ya malalamiko kufuatia uamuzi wa Serikali juu ya eneo hilo.
Amesema katika tume hizo mbili atakazoziunda moja itachunguza na kutoa mapendekezo kuhusu masuala ya ardhi yanayolalamikiwa na wakazi wa Ngorongoro na nyingine itaangakia itekelezaji wa zoezi zima la uhamiaji kwa hiari kutoka eneo la hifadhi ya Ngorongoro.
Rais Samia amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea Kuimarisha Utendaji kazi wa Mamlaka ya eneo la Ngorongoro(NCAA) kwa lengo la Kuimarisha Mahusiano kati ta Serikali na Jamii hiyo.
Vilevile amesisitiza Ulazima wa Wananchi Kushirikishwa ipasavyo katika Upangaji na Utekelezaji wa Miradi inayopita kwenye Maeneo yao.
Aidha Dkt.Samia amesisitiza kuwa Tanzania inayojivunia umoja wa Kitaifa na yenye Serikali inayowahudumia Watanzania Wote.Hivyo ameitaka Ofisi ya Rais Tamisemi Kushugulikia Changamoto zinazojitokeza ikiwemo Kukosekana kwa baadhi ya huduma za Msingi za Kijamii katika eneo la Ngorongoro.