Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Solar Freezer Zinavyoweza Kusaidia Kupunguza Upotevu na Kuharibika Kwa Mazao ya Chakula Baada ya Mavuno



Na Emmanuel Chibasa

Tanzania  sawa na nchi nyingine zinazoendelea Duniani, inakabiliwa na upotevu mkubwa wa mazao kati ya asilimia 20 hadi 30 ya mazao ya mkulima, hupotea baada ya mavuno kutokana na wakulima kuwa na uelewa mdogo wa uhifadhi na matumizi ya teknolojia nafuu na safi kama vile nishati ya jua kwa ajili ya kuhifadhi mazao.

Upotevu wa chakula kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO), hutokea kuanzia shambani baada ya mavuno bila kujumuisha mauzo. Upotevu huo unaweza kufanywa na wakulima, katika mchakato wa uandaaji pamoja na usafirishaji kwa ajili ya uuzaji wa chakula na utupwaji, kwa upande mwingine hutokea sokoni baina ya muuzaji na mtumiaji.

Wakati hali hii ikitokea kwa wakulima hapa nchini na duniani Kwa chakula kupotea baada ya mavuno au kuharibika na kutupwa inakadiliwa kuwa kuna watu takribani Milioni 820 duniani kote wanakabiliwa na njaa.

Shirika la umoja wa mataifa la chakula na kilimo linaeleza kuwa, ni muhimu kuzuia upotevu na utupwaji wa chakula kama mkakati muhimu wa Kukabiliana na athari za mabadiriko ya tabia nchi, kwa kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi lakini pia kuongeza upatikanaji wa chakula, kuchangia uhakika wa chakula pamoja na lishe bora. 

Ukosefu wa elimu ya matumizi ya nishati ya umeme jua na uwekezaji kwenye miradi ya ubunifu ya teknolojia ya nishati ya jua ambayo ni nafuu, safi na uhakika  na inayohamishika kama vile matumizi ya Solar Freezer katika kuhuifadhi mazao ya wakulima wadogo baada ya mavuno, ni sababu kubwa zinayotajwa kuchangia uwepo wa tatizo la ukosefu wa usalama wa chakula na upotevu wa chakula baada ya mavuno.

Ubunifu wa solar freezer ni moja ya suluhisho inayoweza kuwasaidia na kuwawezesha wakulima wadogo na wajasiliamali katika wilaya ya Musoma na mkoa wa Mara kwa ujumla, kupunguza upotevu wa mazao ya chakula baada ya mavuno, na kukuza thamani ya mazao, hivyo kuongeza mapato kwa wakulima lakini pia kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kutokana na upoteaji wa chakula.

Licha ya ukosefu wa elimu na miradi ya nishati ya umeme jua Kwa ajili ya kuhifadhi mazao baada ya mavuno lakini wakulima hao na wawekezaji wanaweza kujifunza jinsi teknolojia hiyo inavyofanya kazi katika maeneo mengine Ikiwa ni pamoja na nchi ya Kenya ambapo Mradi wa solar freeze ulionzishwa Mwaka 2015 mpaka Leo unaendelea kuwahudumia wakulima Wadogo kama Mkakati wa kutatua upotevu wa mazao ya chakula baada ya mavuno. 

MRADI WA SOLAR FREEZE KENYA

Dysmus Kisilu ni mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa solar freeze mradi ambao unatoa suluhisho la upotevu wa mazao ya chakula kwa wakulima wadogo na wafanyabiashara hususani wanawake na vijana nchini Kenya 

Katika taarifa za yake kupitia ripoti ya utafiti wa matumizi ya solar freeze iliyochapishwa na shirika la Equtor Initiative, Dysmus anasema mradi wa solar freeze ni ubunifu wa vyumba vya umeme jua nchini Kenya ambavyo wakulima wadogo wanatumia kuhifadhi mazao mapya kwa kupunguza joto.

Anasema ubunifu  wa teknolojia hiyo ya vyumba vya baridi, unasaidia kuzuia ukuaji wa vijidudu, kupanua ukomo wa maisha ya matunda na mboga mboga kulingana na aina ya mazao kwa Kipindi cha kuanzia siku mbili (2) hadi nne (4) na imekua suluhisho kubwa kwa wakulima wa maeneo ya vijijini sehemu ambazo hazina umeme wa gridi.

Ameongeza kuwa miongoni mwa mafanikio ya mradi huo ni pamoja na kuwafikia wanawake na vijana wengi Wenye umri kuanzia miaka 18-29 ambao kwa Sasa wanamiliki na Kuendesha biashara ndogo ndogo na Kutoa mafunzo ya uendeshaji, matengenezo na utunzaji wa kiufundi wa vifaa vya umeme jua.

Pia kupunguza upotevu wa mazao mapya baada ya mavuno kwa Asilimia 90 pamoja na kuwafikia wakulima wadogo 3,000 ambao wananufaika Moja Kwa Moja huku pia ukisaidia uwezeshaji wa Kijinsia takribani Asilimia 80 au wakulima 2,400 ambao ni wanawake 

HALI YA KILIMO NA UMASIKINI WA CHAKULA

Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 katika ripoti ya hali ya usalama wa chakula kwa Tanzania bara, kulingana na takwimu  za utafiti wa mapato na matumizi  ya kaya binafsi mwaka 2017-2018 ya ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania (TBS) iliyotolewa September 2024 inaonesha kuwa, Sekta ya kilimo inachangia pato la taifa kwa asilimia 26.5, asilimia 63.4 ya kaya zinajishughulisha na kilimo na asilimia 26.4 ya watu wa Tanzania bara wana umasikini wa mahitaji ya msingi, wakati asilimia 8.0 ya watu wanaishi katika umasikini wa chakula. 

Shirika la chakula na kilimo la umoja wa mataifa (FAO) linakadiria kuwa, takribani theluthi moja ya chakula chochote kinachozalishwa ulimwenguni hupotea au kuharibika na athari za mazingira ni kubwa, ikiwa ni hekta bilioni 1.4 za ardhi, karibu asilimia 30 ya eneo la ardhi ya ulimwenguni linazalisha chakula ambacho hakijaliwa.

Tatizo hili linatokana na mifumo mingi ya kilimo cha chakula duniani kutokua endelevu na inaharibu ardhi ya kilimo, inachangia uzalishaji wa gesi chafuzi na upotevu wa bioanuwai na hutumia maji mengi ya ardhini.

MATUMIZI YA NISHATI KWA WAKULIMA MUSOMA

Wakati matumizi ya nishati ya jua Kupitia Mradi wa solar freeze yakionesha kuwasaidia wakulima Nchini Kenya na Kusaidia kupunguza upotevu wa mazao ya chakula baada ya mavuno lakini hali ni tofauti Kwa wakulima katika wilaya ya Musoma na Mkoa wa Mara Kwa ujumla.

Inaelezwa kuwa ukosefu wa elimu ya nishati  ya umeme jua pamoja na kutokuwepo kwa miradi ya umeme jua bado wakulima wadogo na Jamii Kwa ujumla, hawana uelewa wa kutosha juu ya faida za teknolojia hii, huku changamoto nyingine ikitajwa kuwa gharama kubwa za vifaa zinapelekea watu wengi kushindwa kumudu kununua kutokana na hali ya maisha.

Butilikwa Lazaro ni afisa kilimo mkoa wa Mara, anasema ukosefu wa elimu ya matumizi ya teknolojia ya nishati ya umeme jua katika kuhifadhi mazao ya chakula kwa kutumia Solar Freezer baada ya mavuno kunachangia pakubwa kwa wakulima kuendelea kuathirika licha ya kuendelea kujishughulisha na shughuli za kilimo.

Amesema pia kukosekana kwa miradi ya teknolojia ya umeme jua katika kuhifadhi mazao baaada ya mavuno kwa kutumia Solar Freezer katika mkoa wa Mara, pia kunachangia kukwamisha wakulima na wawekezaji kukosa kujifunza jinsi teknolojia hiyo inavyofanya kazi na kama serikali inaendelea na mkakati wa kuhamasisha matumizi ya nishati jadidifu ikiwa ni pamoja na matumizi ya umeme jua katika shughuli mbalimbali za kilimo.  

“ Ni kweli wakulima wadogo katika mkoa wa Mara wanakabiliwa na tatizo la upotevu wa chakula baada ya mavuno, na hii inatokana na ukosefu wa elimu juu ya matumizi ya teknolojia ya umeme jua katika kuhidhadhi chakula baada ya mavuno ili kisiharibike na tunaendelea kuhamasisha matumizi nishati mbadala kwa wakulima.

Katika mkoa wetu pia hatuna uwekezaji kwenye mradi wa umeme jua kwa ajili ya kuwasaidia wakulima wadogo kuhifadhi mazao yao, nitoe rai kwa wawekezaji wasaidie kuwekeza pia katika eneo hili ili kutatua changamoto hii kwa wakulima katika mkoa wetu, ” amesema Butilikwa. 


UELEWA WA WAKULIMA NA WAFANYABIASHARA

Uchunguzi wa George Marato Tv katika mahojiano na baadhi ya wakulima na wafanyabiashara umebaini kuwa, bado uelelewa wa matumizi ya nishati ya umeme jua katika kuhifadhi chakula kwa kutumia Solar Freezer uko chini, huku baadhi yao wakiwa na uelewa wa solar kwa ajili ya kupata mwanga na kuchaji simu pekee.

Sara John mkazi wa musoma na muuzaji wa mboga mboga na matunda anasema hajawahi kuiona au kusikia kuhusu Solar Freezer inavyoweza kutumika kuhifadhi mazao ili yasiharibike baada ya mavuno.

“Nimekua nikinunua mboga mboga na matunda toka kwa wakulima kwa kiwango kidogo ili kutosheleza matumizi ya muda mfupi na nimekua nikiweka mboga mboga kwenye chombo nilichoweka maji ili zisiharibike kwa haraka, ” Amesema Sara. 

Peter Marwa, mkulima wa mboga mboga na matunda, anasema katika maeneo ya vijijini hajawahi kuona wakulima wanatumia solar freezer lakini amekua akiziona freezer za kawaida Zinazotumia umeme kwa wafanyabiashara wa maduka na pia kwa wanaohifadhi samaki Kwa ajili ya kusafidisha.

“Ningependa kujua hizo freezer zipo kama hizi za kawaida au zenyewe zipo tofauti? moja inaweza kuhifadhi mazao kiasi gani na kwa wakulima wangapi nikipewa elimu hiyo itanisaidia sana kupata uelewa wa matumizi yake ” Anasema Peter. 

Naye Magdalena Ogutu mkazi wa Musoma  ambaye ni mkulima wa nyanya pamoja na mume wake, anasema kuwa katika mtumizi ya solar anafahamu juu ya kupata mwanga, kuchaji simu pamoja na kumwagilia na freezer anazozifahamu ni zile zinazotumia umeme wa kawaida.

“Hatujapewa elimu ya hizo freezer kama wakulima katika kuhifadhi mazao yetu, nahitaji kufahamu upatikanaji wake tunapata wapi na gharama zake zikoje  sababu vifaa Vya solar kidogo vina gharama” Anasema Magdalena.

Naye James Obare, mkulima wa mahindi na maharage, anasema kutokua na ufahamu wa teknolojia hiyo kunasababisha wakulima kupoteza mazao baada ya mavuno sababu hawelewi jinsi gani teknolojia hiyo inavyoweza kuwasaidia.

“Unasema inaweza kuhifadhi mazao wakati wa mavuno  na baada ya mavuno, lakini hatujawahi kufundishwa wala kuona mfano wake, ingekuwa vizuri kama wangeleta hapa vijijini kwetu ili tujifunze,” anasema James.

MIKAKATI YA SERIKALI NA WADAU

Katika Kukabiliana na tatizo la upotevu wa chakula baada ya mavuno, Serikali kwa kushirikiana na shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) inatekeleza mradi wa miaka mitano wa Feed the Future Tanzania wenye thamani ya shilingi bilioni 60 (Dola za kimarekani milioni 24) kama mkakati wa kupunguza upotevu wa chakula baada ya mavuno katika mnyororo wa thamani ya kilimo cha mboga mboga na nafaka nchini Tanzania. 

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa  Katika Ziara Marekani tarehe 30 October, 2024 Katika mji wa Des Moines, Iowa, alielezea dira yake ya kuifanya Tanzania kuwa mzalishaji mkubwa wa chakula barani afrika kupitia mikakati mitatu mikuu ya Serikali katika sekta ya kilimo ambayo ni

1. Uwekezaji katika Miundombinu ya Umwagiliaji: Serikali imepanga kuwekeza katika miradi mikubwa ya umwagiliaji ili kuhakikisha ardhi nyingi zaidi inakuwa na uwezo wa kuzalisha mazao kwa mwaka mzima. Hii inalenga kuongeza uzalishaji wa chakula na kupunguza utegemezi wa mvua.

2. Kuboresha Upatikanaji wa Teknolojia na Pembejeo za Kisasa: Ili kuongeza tija na ubora wa mazao, Serikali inashirikiana na wadau wa maendeleo kutoa teknolojia za kisasa na pembejeo kwa wakulima. Hii itasaidia wakulima kuongeza uzalishaji na kupata mazao bora yenye thamani kubwa kwenye masoko ya ndani na nje.

3. Kukuza Masoko ya Mazao ya Kilimo: Serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha mazao yanayozalishwa nchini yanapata masoko ya ndani na nje, na hivyo kuwapa wakulima faida zaidi kutokana na juhudi zao.

Rais Dkt. Samia alieleza kwamba kwa mikakati hii, Tanzania inaweza kuwa mzalishaji mkubwa wa chakula barani Afrika na hivyo kuchangia zaidi kwenye usalama wa chakula katika kanda nzima.

Mbali na Mikakati hiyo ya serikali pia shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO ) na Benki ya Dunia kwa pamoja zinapanga mipango ya sekta ya mavuno, ikiwa ni pamoja na uhifadhi kwenye baridi, kusafisha, kupanga, na kufunga hatua za uzalishaji, itatoa asilimia 47 ya dola bilioni 940 katika uwekezaji unaohitajika kumaliza njaa katika nchi za kusini mwa jangwa la sahara ifikapo 2050.

Utumiaji wa solar freezer unaweza kusaidia kufanikisha malengo kadhaa ya maendeleo endelevu (SDGs) ya ajenda ya 2030 namba 1,2,5,7 pamoja na 13.

Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...