Mwanariadha wa Jeshi la Polisi, Konstebo Transfora Mussa amekuwa mshindi wa kwanza wa mbio za kilometa 10 za Fulham upande wa wanawake zilizofanyika nchini Uingereza Novemba 17, 2024, huku akivunja rekodi ya kukimbia muda mfupi zaidi.
Transfora ambaye alipewa medali ya dhahabu, amevunja rekodi hiyo kwa kutumia muda wa dakika 31:53 tofauti na rekodi ya mwaka jana, ambapo mwanariadha kutoka nchini Kenya alishinda kwa kutumia muda wa dakika 33:11 katika mashindano hayo.

Comments
Post a Comment