Na Ada Shadrack;Musoma.
MWANYA wa rushwa umetajwa kuwa kichocheo cha kushinda uchaguzi wa kura za maoni kwa baadhi ya wagombea nafasi ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa Mjini Musoma mkoani Mara.
Hayo yamebainishwa na aliyekuwa mgombea nafasi hiyo kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (ccm) kata ya kitaji 'A' mzee Ally Z. Rajabu wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Mzee Ally z. Rajabu amesema uchaguzi huo umefanyika octoba 23 mwaka huu ambapo mgombea mwenzake Salma Ally alipata kura 97 akawa wa kwanza na kwamba yeye alipata kura 91 na kushindwa kinyang'anyiro hicho.
Aidha baada ya kushindwa kupata nafasi hiyo Ally Z Rajabu aliamua kuhama chama hicho na kwenda chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) huku akiwa na nia ya kugombea tena nafasi hiyo kupitia chama hicho.
" Baada ya kukaa na kulinganisha vyama mbalimbali nikaapa sitakuwa na tajiri yoyote wa kumtegemea kunipa nguvu ya fedha ili nishiriki uchaguzi sipendi kabisa yawezekana pesa inaweza kunisaidia kuchaguliwa lakini kumbe sikuwa chaguo sahihi " amesema.
Kwa upande wake diwani wa kata hiyo Golden Charles kupitia chama cha chadema alimpokea kwa furaha na bashasha kubwa na kumuhahidi kushirikiana naye katika shughuli za maendeleo ya wananchi.
" Tunamkabidhi kadi ya uanachama wa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) pamoja na fomu ya kugombea nafasi ya uenyekiti wa serikali ya mtaa wa kitaji A. alisema Golden.
Pia aliwataka baraza la wazee la kata hiyo kuungana na mwanachama huyo mpya na kushirikiana nae kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo kwakuwa wazee husifika kuwa na busara na hekima.
Akijibu tuhuma za uwepo wa rushwa kwenye uchaguzi huo , mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (ccm) kata hiyo ya kitaji Wambura Mtete alisema hakuna malalamiko ya tuhuma zilizofikishwa katika ofisi hiyo vinginevyo uchaguzi ulifanyika kwa kuzingatia taratibu na miongozo ya chama hicho.



