Rais Mwinyi achangia millioni 100 ukarabati wa kanisa katoliki Zanzibar

GEORGE MARATO TV
0



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi  amesema Serikali itaendelea kuimarisha Uhuru wa Kuabudu  na  kuziagiza taasisi za Kidini kuendelea kuiombea nchi Amani na Umoja.

 Rais Dk,Mwinyi amefahamisha kuwa  taasisi za Kidini  zina wajibu mkubwa wa kushirikiana na Serikali  na kuunga  Mkono  juhudi za  kuleta Amani,Umoja  na Mshikamano  wa Watanzania.

Rais Dk, Mwinyi  ameyasema hayo leo tarehe 27 Oktoba 2024 alipozungumza  katika Maombi maalum  ya kumpongeza Askofu Agustino Shao  kwa utume wake  katika Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar  na  maombi kwa Taifa  iliyofanyika Viwanja vya Mao Tse Tung Mkoa wa Mjini Magharibi.

Rais Dk , Mwinyi  amesisitiza kuwa Serikali inathamini mchango mkubwa unaotolewa na Kanisa katoliki Jimbo la Zanzibar   kwani  umekuwa msaada muhimu  wa kuimarisha  ustawi wa jamii katika nyanja mbalimbali.

Akizungumzia  ukarabati wa Kanisa la Minara miwili unaotarajiwa kutekelezwa na Kanisa hilo  kuwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali na shirika la Elimu Sayansi na Utamaduni la Umoja wa mataifa UNESCO la kuimarisha Mji Mkongwe wa Zanzibar ambao ni Urithi wa Dunia.

Hali kadhalika Rais Dk.Mwinyi  amechangia shillingi Millioni Mia moja na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk, Samia Suluhu Hassan amechangia shilingi Milioni 50 kwa ajili ya Ukarabati wa Kanisa la Mtakatifu Joseph liliopo Shangani Wilaya ya Mjini.

Kwa upande mwingine Rais Mwinyi amewasisitiza  Waumini wa Kanisa Katoliki  kuendelea kuiombea  nchi Amani kwani ni nguzo muhimu ya kuleta Umoja ,Amani na Upendo  jambo linaloifanya nchi kupiga hatua kubwa za  Maendeleo.







Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top