Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Mhe.Ghati Zephania Chomete, Leo tarehe 27 Septemba 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Balozi Dkt.Emmanuel John Nchimbi.
Mhe.Ghati ametumia fursa hiyo kumpongeza Balozi Dkt.Nchimbi kwa namna anavyosimamia shughuli za Chama, Jumuiya na Idara zake kama Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi kwa ngazi ya Taifa.
Mhe.Ghati amemhakikishia Dkt.Nchimbi kuwa wanawake na wananchi Mkoani Mara wataendelea kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kumpa kura za ndio na za kishindo katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika novemba mwaka huu pamoja na uchaguzi mkuu wa mwakani kutokana na Utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo.