Wana Ruangwa Kumpa Zawadi Kubwa Rais Dkt. Samia 2024-2025

GEORGE MARATO TV
0

 



WANANCHI wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, wamesema zawadi pekee ya kumlipa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo katika jimbo hilo, ni kushinda uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Wamesema wamejipanga kushinda vitongoji na vijiji vyote tisini  vya jimbo hilo katika uchaguzi huo wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu .

Akizungumza baada ya mapokezi makubwa na ya aina yake katika viwanja vya madini jimbo la   Ruangwa katika siku ya Hamasa maarufu kama HAMASA DAY, ambayo imeshirikisha vijana wa CCM wa kata 22 za jimbo hilo,mbunge wa Ruangwa ambaye pia ni waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa,amesema Rais Samia,ametoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika jimbo hilo.

Amesema hivi sasa kata 22 zina shule za Sekondori na huku baadhi zikiwa na shule zaidi ya moja huku Rais Samia akitoa fedha zaidi za ujenzi wa shule tatu sekondari kwa wanafunzi wa kike kwa masomo ya Sayansi na chuo cha ufundi jimboni humo.

Hata hivyo amesema pamoja na kumpa zawadi hiyo ya ushindi kwa ngazi za vitongoji na vijiji pia Wana Ruangwa wamejipanga kuhakikisha katika uchaguzi mkuu, Rais Samia anapata kura za kishindo katika jimbo hilo na kwamba msimamo wa Wana Ruangwa ni fomu moja kwa Rais Samia.

Hata hivyo ametumia nafasi kusema 2025 nia yake ya kugombea ubunge jimbo hilo ipo pale pale kwani bado ana nguvu na uwezo mkubwa wa kuwatumikia wana Ruangwa.

Ametumia mkutano huo wa HAMASA DAY kuwashukuru wananchi wa jimbo la Ruangwa wa ndani na nje kwa ushirikiano wao mkubwa na kuchangia kasi ya maendeleo ya jimbo hilo.

Amesema hata vyama rafiki ya CCM wamekuwa na ushirikiano mzuri katika suala la maendeleo ya jimbo hilo.

Mgeni Rasmi katika siku hii ya Hamasa ya vijana wa CCM jimbo la Ruangwa ni mwenyekiti wa umoja wa vijana wa CCM  Taifa Mohamed Kawaida,ambaye amesema kwa hamasa hiyo lazima ccm iibuke ushindi mkubwa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.

Mwenyekiti huyo wa umoja wa vijana taifa amesisitiza vijana kudumisha mshikamano na umoja wakati wote na kwamba atakuwa mstari wa mbele kutetea kundi hilo katika jamii

Katika siku hii ya hamasa kwa vijana wa CCM  jimbo la Ruangwa,mbali na kupambwa na wasanii mbalimbali,kikiwemo kikundi cha Sanaa cha TOT,kikundi cha wakina Mama cha galaula kikiwa kivutio kikubwa katika siku hii.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top